Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Miss Ukonga na Miss Tabata wafanya mazoezi ya pamoja

Miss Ukonga na Miss Tabata wafanya mazoezi ya pamoja



 Miss Ukonga 2012 walio chuchumaa wakiwa
katika picha ya Pamoja na wartembo wa Miss Tabata 2012 wakati
walipofanya mazoezi ya pamoja jana. 
  
WAREMBO
wa vitongoji viwili vya Ukonga na Tabata jana walifanya mazoezi ya pamoja
katika kuleta ushirikiano na kujenga urafiki baina ya warembo hao katika fani
ya urembo.
Warembo
wa Tabata waliwatembelea wenzao wa Ukonga katika kambi yao ya mazoezi iliyopo
Ukonga Hill Tech Bar maeneo ya Minazi Mirefu au maarufu Banana.

Vitongoji
vya Ukonga na Tabata warembo wake watakao shinda wanataraji kukutana katika
Kambi ya kanda ya Ilala kabla ya kwenda kushiriki shindano la taifa la Miss
Tanzania 2012.

Wakizungumza
jana baadhi ya warembo wa Ukonga wamesema ushirikiano wao huo na wenzao wa
Tabata unawapa uwezo wa kijiamini na kupata nafasi ya kujifunza kile ambacho
wenzao wanakifanya au wamejifunza ikiwa ni pamoja na utembeaji, uongeaji wa
kati wa kujitambulisha na vitu vingine vingi.

“Tunawashukuiru
sana waandaji wetu, maana mbali ya kuwa tunapata wageni wa aina mbalimbali
ambao ni wadau wa urembo lakini leo tupo na washiriki wenzetu wa tabata ambao
tunaimani tutakutana katika shindano la Ilala”, alisema Amina Sangawe.

Nae
Suzanne Deodatus ambaye ni Mshiriki kutoka Tabata alisema wamepata fursa ya
kujifunza mambo kabdhaa na wamefurahi sana kuwatembelea warembo wa Ukonga na
kufnya nao mazoezi ya pamoja.

Mapema
Mwezi huu warembo wa Ukonga waliwasindikiza Miss Tabata 2012 katika show yao
kubwa ya Utambulisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar West Tabata.

Shindano
la Miss Ukonga 2012 linataraji kufanyika Mei 5, mwaka huu na lile la Tabata
linataraji kufanyika mapema mwezi Juni.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa