Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA KUPIGWA PICHA ZA UCHI WAKATI WA TAMASHA LA FIESTA DODOMA.

WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA KUPIGWA PICHA ZA UCHI WAKATI WA TAMASHA LA FIESTA DODOMA.



Msaanii maafuru wa filamu nchini Tanzania asiyeishiwa na vibweka Wema Sepetu (katikati) akizungumza na wanahabari katika ukimbi wa habari maelezo jijini Dar kwa nia ya kuomba radhi kwa watanzania kwa niaba yake na msanii mwenzake Ant Ezekiel kuhusiana na tukio la wao kupigwa picha zilizowaonyesha ‘ndivyo sivyo’ nusu uchi wakati wakijiachia katika Tamasha la Serengeti Fiesta lilipofanyika mkoani Dodoma. Kulia ni Msanii wa Bongo Movie Ant Ezekiel na kushoto Katibu Mkuu wa TAFF Wilson Makubi.
Msanii Maarufu wa filamu za Bongo Ant Ezekiel akisisitiza kuwa wao wameoumia sana kwa kuonekana kwa picha zile kwa sababu wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi. Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na mashabiki mbalimbali wa kazi zao ambao wanawaheshimu kuliko baadhi ya watu wanavyofikiria.
Wema Sepetu Mbele ya kamera ya MO Blog akiomba radhi na kusema watanzania “ Kiukweli hatujafurahia na tumeumia sana” na tunatumia fursa hii kuomba Msamaha.
Moja ya picha ya Msanii Aunty Ezekiel iliyosamba kwenye mitandao ya Kijamii hivi karibuni wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa