Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Hoteli ya kitalii Ikondolelo Lodge iliyoko Kibamba Jijini Dar es salaam , Imeteuliwa kuwa Kambi Rasmi ya warembo Mwaka huu 2012.

Hoteli ya kitalii Ikondolelo Lodge iliyoko Kibamba Jijini Dar es salaam , Imeteuliwa kuwa Kambi Rasmi ya warembo Mwaka huu 2012.


Hoteli ya kitalii Ikondolelo Lodge iliyoko Kibamba Jijini Dar es salaam ,Imeteuliwa na Bodi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania kuwa Hotel Rasmi ya mashindano hayoMwaka huu 2012.
Mchakato wa uteuzi ulihusisha Hotel zaidi ya saba zilizojitokeza kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012.
Kwa Ikondolelo kuwa hotel Rasmi Miss utalii Tanzania itatumia zaidi ya Shilingi za kitanzania Milioni mia moja ,ikiwa ni udhamini wa gharama za kambi ya Warembo na waandaaji zaidi ya sitini (60) kwa muda wa wiki tatu.

Bodi katika kuteua hotel rasmi ya mashindano mwaka huu imezingatia Vigezo vifuatavyo: Usalama wa watu na mali zao, ubora wa viwango vya huduma ambayo siyo chini ya hadhi ya nyota (3) ,mazingira ya hotel na utulivu wa eneo husika kulingana na viwango vya kitaifa na Kimataifa vya mashindano ya Miss Utalii, pia kwakuzingatia viwango vilivyowekwa na serikali kupitia Baraza la sanaa la Taifa (BASATA).
Warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na Vyuovikuu, wakiwa kambini katika Hotel ya Ikondolelo watafanya shughuli mbalimbali za maandalizi na kijamii; zikiwemo, Kujifunza kuogelea katika bwawa lililopo hotelini hapo, Upigaji wa picha za minato katika bustani zinazozunguka hoteli,watapewa mafunzo maalum ya kutumia maeneo na vifaambalimbali vya hotel za kitalii. Aidha washiriki wa fainali za taifaza Miss utalii 2012 watapewa mafunzo kuhusiana na utalii, utamaduni, uwekezaji, mazingira, afya ya jamii, elimu ya jamii uzalendo, watafundishwa mbinu za kujieleza, kujiamini na kufanya matangazo.

Mkurugenzi mtendaji wa Ikondolelo Lodge Ndugu Fredy Selekwa ameishukuru Bodi ya Miss utalii Tanzania kwa kuwapa fulsa yakuwa hotel Rasmi ya Mashindano haya muhimu kwa taifa katika kukuza secta ya utalii na uchumi kwa ujumla. Ameihakikishia washiriki na viongozi watakaokuwa kambini kuwapatia huduma zote muhimu kwa kiwango cha kimataifa
Imetolewana
Hamisi .A.Mkongowale
Mratibu wa Matukio

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa