Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » RAIS OBAMA WA MAREKANI ATUA SALAMA TANZANIA

RAIS OBAMA WA MAREKANI ATUA SALAMA TANZANIA




Rais wa Marekani Barack Obama akifurahia ngoma za utamaduni mara baada ya kutua nchini Tanzani katika jiji la Dar es salaam 

Wadadisi na wachambuzi wa masuala ya Kiuchumi na kisiasa wanaeleza kuwa ziara ya Rais Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na
 China katika uhusiano wao na Afrika.
Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili katika ardhi ya Tanzania muda huu katika ratiba yake ya mwisho wa ziara  barani Afrika.
Wadadisi na wachambuzi wa masuala ya Kiuchumi na kisiasa wanaeleza kuwa ziara ya Rais Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.
Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.
Baadaye Rais Kikwete amemuongoza Rais Obama kuelekea Ikulu ya Tanzania kwa ajili ya shughuli zingine zilivyopangwa.
Chanzo Gazeti la Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa