Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » ASKARI MAGEREZA ALIYEFARIKI KWA AJALI MKURANGA AAGWA UKONGA DAR

ASKARI MAGEREZA ALIYEFARIKI KWA AJALI MKURANGA AAGWA UKONGA DAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

photoKamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Deonice Chamulesile akiwaongoza Mamia ya Waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo aliyefariki kwa ajali ya gari Aprili 22, 2014 majira ya saa Saba mchana wakati akisindikiza Mahabusu kutoka Mahakama ya Mwanzo Kimanzichana Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Katika ajali hiyo pia walikufa Mahabusu wanne waliokuwa wanatoka kusikiliza kesi zao.2 (1)Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakiaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo katika Kambi ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam leo Aprili 24, 2014.


image (5)Mke wa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo akisaidiwa na mmoja wa Waombolezaji kumuaga Mme wake aliyefariki kwa ajali ya gari.
4Mmoja wa ndugu wa Marehemu akiwa amebebwa na Waombolezaji baada ya kuzimia katika tukio la kuaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza Peter Shelukindo.
5Baadhi ya Waombolezaji walijitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza Peter Shelukindo aliyekufa kwa ajali ya gari Wilayani Mkuranga(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa