Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » CWT:MSIMAMO WETU NI SERIKALI TATU

CWT:MSIMAMO WETU NI SERIKALI TATU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Rais wa CWT,Gratian Mukoba
 
Chama  cha Walimu nchini (CWT), kimesisitiza kuwa msimamo wake ni muundo wa serikali tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema Chama cha Walimu Tanzania mwishoni mwa mwaka jana kikiwa kama Taasisi Huru, kilikaa kama Baraza la Katiba na kuazimia juu ya Muundo wa Muungano wa Serikali tatu.

Alisema baada ya Mkutano Mkuu kupitisha kwa kauli moja Oktoba, mwaka jana, alipeleka maoni yao kwenye ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuyakabidhi.
                                                                
“Tuliposikia rasimu ya pili imetoa maoni hayo, tuliridhika kuwa maoni yetu yamekubalika,” alisema.

Aidha, Mukoba alisema CWT kama zilivyo taasisi nyingine, kina wanachama wengi wenye mitazamo tofauti, lakini kikifikia makubaliano katika mambo ya msingi, lazima maoni ya taasisi yawekwe mbele, na maoni binafsi yahifadhiwe moyoni.
 
Alisema kama kuna mwanachama mwenye maoni binafsi yanayotofautiana na hayo ya CWT, basi anapaswa kuweka bayana kwamba ni yake binafsi na si msimamo wa chama hicho.

Msimamo huo wa chama hicho unatokana na taarifa zilizotolewa na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiunga mkono msimamo wa serikali mbili wakati wakijua kwamba hayo ni maoni yao binafsi na wala si msimamo wa chama hicho.

“Juzi tukiwa Tanga kwenye Baraza la CWT lililokaa tarehe 15-16 Aprili, 2014, wajumbe walisisitiza msimamo wao juu ya Muundo huu wa Serikali tatu na kuniagiza niongee na vyombo vya habari ili kuuweka wazi.

"Kwa kuwa mimi ndiye msemaji wa CWT, narudia tena kusema kuwa msimamo wetu juu ya Muundo wa Muungano ni ule wa Serikali tatu,” alisisitiza.

Alisema wanaamini katika Muungano wa kweli na kwamba  haiwezekani mtu akaishi amefunga geti la nyumba yake na akiulizwa kwa nini huwa halifunguliwi akajibu kuwa anahofia mke wake ataondoka.

“Mke au mume anatakiwa kutoka na kurudi nyumbani bila kuwekewa shinikizo la kufungiwa geti,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa