Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KESI YA USAMBAZAJI ARV's FEKI:MAELEZO YA AWALI KUSIKILIZWA MEI 14

KESI YA USAMBAZAJI ARV's FEKI:MAELEZO YA AWALI KUSIKILIZWA MEI 14

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Ramadhani Madabida
 
Maelezo  ya awali dhidi ya kesi inayomkabili Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano, ya usambazaji wa dawa bandia za Kupunguza Makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) na kuisababishia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) hasara ya zaidi ya Sh. milioni 148.3, yatasikilizwa Mei 14, mwaka huu.
Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Nyigulila Mwaseba.

Hakimu Mwaseba alisema dhamana ya washtakiwa inaendelea.

Madabida ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa wa kiwanda cha kutengeza dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPIL), anashtakiwa pamoja naye, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa Dawa wa MSD, Sadiki Materu na Meneja Uendeshaji, Seif Shamte.

Wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Meneja Masoko, Simon Msoffe, Mhasibu Msaidizi wa MSD, Fatma Shango na Evans Mwemezi.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi, ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 10, mwaka huu na washtakiwa kwa nyakati tofauti walipata dhamana.

Awali, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Faraja Nchimbi, akisaidiwa na Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro, uliwasomea mashitaka hayo.

Pamoja na mashitaka mengine, Madabida, Shamte, Msoffe na Shango, wanadaiwa kwamba, Aprili 5, mwaka 2011, jijini Dar es Salaam, waliuza na kuisambazia MSD makopo 7,776 ya dawa bandia aina ya Antiretroviral.

Kimaro alidai washitakiwa hao walifanya hivyo kuonyesha kuwa dawa hizo ni halisi aina ya ‘Antiretroviral’ wakati wakijua siyo kweli.

Pia wanadaiwa kuwa wakiwa na nyadhifa zao hizo, waliisambazia MSD makopo 4,476 ya dawa aina ya ‘Antiretroviral’.

Alidai dawa hizo zinajumuisha gramu 30 za ‘Stavudide’, gramu 200 za ‘Nevirapine’ na gramu 150 za ‘Lamivudine’ zenye ‘Batch’ namba OC 01.85 zikionyesha zimezalishwa Machi, 2011 na kuisha muda wake Februari, 2013.

Kimaro alidai kuwa washitakiwa hao walifanya hivyo kwa lengo la kuonyesha kuwa dawa hizo ni halisi aina ya ‘Antiretroviral’ wakati wakijua siyo kweli.

Kimaro alidai washitakiwa hao wanadaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati ya Aprili 5 na 13, mwaka 2011, jijini Dar es Salaam, wakiwa kama waajiriwa wa  MSD kama Meneja Udhiditi Ubora na Ofisa Udhibiti Ubora, walishindwa kutumia nyadhifa zao kudhibiti kosa hilo lisitendeke.

Washtakiwa wote walikana mashitaka hayo na upande wa Jamhuri ulidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa