Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KIGOGO TANESCO ASHTAKIWA KWA KUISABABISHA SERIKALI HASARA YA MIL.200/-

KIGOGO TANESCO ASHTAKIWA KWA KUISABABISHA SERIKALI HASARA YA MIL.200/-

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
 
Aliyekuwa  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Semtutu na wenzake wanne, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka mawili yakiwamo ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. milioni 200.
Washtakiwa wengine  katika kesi hiyo ni  aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa Fedha, Lusekeo Kasanga, Mwanasheria Godson Ezekiel  na Mkandarasi Martin Abraham.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isdore Kyando alidai kuwa  washtakiwa walifanya makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011.

Kyando alidai kuwa katika shitaka la kwanza, Desemba, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo jijini Dar es Salaam washtakiwa  walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha  Mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa