Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZAHARIBU MIUNDOMBINU YA RELI KWA NJIA YA DAR ES SALAAM-TANGA-MOSHI KATIKA ENEO LA MING'ONGO KILOMITA 4 KUTOKA STESHENI YA RUVU

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZAHARIBU MIUNDOMBINU YA RELI KWA NJIA YA DAR ES SALAAM-TANGA-MOSHI KATIKA ENEO LA MING'ONGO KILOMITA 4 KUTOKA STESHENI YA RUVU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Sehemu ya njia ya reli katika eneo la Ming’ongo ikiwa inaning’inia baada ya tuta kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kipalo Amani Kisamfu pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo mchana kuona athari kubwa iliyotokea kwenye njia ya reli. Aidha, katika njia hiyo kilomita kumi na nane za njia ya reli zimeaharibiwa na mvua hizo zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Reli, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Festo Mwanjika (wa pili kutoka kulia) akiangalia uharibifu mkubwa uliotokea kwenye njia ya reli katika eneo la Ming’ong’o kilomita 4 kutoka Stesheni ya Ruvu, alipotembelea eneo hilo kujionea moja kati ya sehemu kumi na nane zilizoharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Uchukuzi)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa