Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » NCHEMBA AOMBA JK ASHAURIWE UTEUZI WAJUMBE 201

NCHEMBA AOMBA JK ASHAURIWE UTEUZI WAJUMBE 201

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwigulu Nchemba
 
Mwenyekiti  wa Bunge Maalumu la Katiba ameombwa kumshauri Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa wajumbe wa kundi la 201 waliosusia kikao cha juzi na kutoka nje.
Ombi hilo limetolewa na mjumbe wa Bunge hilo, Mwigulu Nchemba, alipoomba mwongozo wa mwenyekiti wakati wa uchangiaji wa rasimu ya katiba.

Mwigulu alisema kitendo cha baadhi ya wajumbe hao kuungana na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kususia kikao si cha kiungwana.

Alisema jambo hilo halikutokea juzi, bali lilishapangwa.

“Kumekuwa na hatua mbalimbali zinazoonyesha kuwa hawakutaka mchakato huu wa katiba ufanikiwe,” alisema.

 Alitaja dalili hizo kuwa ni pamoja na kutishia kujitoa katika hatua mbalimbali, ikiwamo ya kutunga kanuni kwa madai kuwa ni lazima wao wapewe nafasi zaidi na walipewa, lakini yote hawakuyathamini.

Alisema Bunge limetumia fedha nyingi za walipakodi kwa ajili ya Bunge hilo ili kupata katiba, lakini wajumbe hao wamesusia Bunge hilo kwa makusudi.

Kwa mujibu wa Mwigulu, fedha hizo zingeweza kufanya kazi nyingine kwa wananchi, ikiwamo kununua dawa, kusomesha vijana na hata kujenga zahanati.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako, hawa ndugu zetu waliotoka na wanatoka katika kundi la 201, ambao wapo katika mamlaka ya uteuzi wa rais ni kwanini basi usimshauri rais atengue uteuzi wao na kuteua wapya?” alihoji.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa