Watoto wa kituo cha Amani Orphanage Centre wakifurahia
baadhi ya vifaa vilivyotolewa na TAS
-
Chama cha Watanzania waishio Geneva wametoa mchango
wa vifaa ikiwa pamoja na tank la kuhifadhia maji,viti na meza
za kusomea, jiko la gesi na mtungi wa Gesi ili kusaidia watoto wa kituo
cha Amani Orphanage Centre. Msaada huo uliwasilishwa kwa niaba ya TAS
na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt Agnes Kijazi.
Akiwasilisha mchango huo kwa niaba ya TAS, Dkt Kijazi alielezea upendo
walionao watanzania hao kwa kuwakumbuka watoto wa kituo cha Amani.
Alisema upendo huo ni mfano wa kuigwa kwa watanzania waishio ndani na
nje ya nchi. Kwa upande wa watoto Dkt. Kijazi aliwahakikishia kwamba
TAS na TMA wanawapenda. Alichukua fursa hiyo kuwakumbusha upendo ambao
umeonyeshwa kwao na wanawake wa TMA kwa kuwasaidia baadhi ya mahitaji
yao.
Aidha Dkt Kijazi alisema TAS wameendelea kuonyesha
moyo wa upendo kwani hivi karibuni wametoa msaada wa fedha (Tshs 500,000)
kwa Mama Aida wa Mbeya aliyejifungua wototo wanne mwanzoni mwa mwaka
huu. Msaada huo uliwasilishwa kwa niaba ya TAS na meneja wa TMA kanda
ya nyanda za juu kusini magharibi Bwana Issa Hamad.
Akipokea msaada huo msimamizi na mwanzilishi wa kituo
cha Amani Bi. Margareth Mwegalawa aliwashukuru watanzania wote
waishio Geneva kwa kuwakumbuka watoto wa Amani hata kuwawezesha kupata
baadhi ya mahitaji waliokuwa wanahitaji, na alimuomba Dkt Kijazi kuwasilisha
salamu hizo kwa kusisitiza msaada huo sio mdogo bali ni mkubwa sana
kulingana na uhitaji wake. Bi. Magreth alisema kituo chicho kina watoto
37 wakiwa wasichana 25 na wavulana 12 wenye umri kati ya mwaka mmoja
(1) na miaka kumi na tano (15).
Akizungumza kwa niaba ya watoto wa Amani Orphanage
Centre mtoto Beatrice Phine alisema sote tunafurahi kwa kupata tank
la maji, viti na meza ambavyo vitaboresha maisha yetu na mazingira ya
kusomea. Alimuomba Dr. Kijazi awafikishie salaam zao za upendo na shukrani
kwa TAS.
0 comments:
Post a Comment