Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Wiki ya chanjo Afrika kuzinduliwa kesho

Wiki ya chanjo Afrika kuzinduliwa kesho

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mratibu wa Chanjo Zanzibar Bw. Yusuf Haji Makame akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu wiki ya chanjo Afrika itayozinduliwa kesho na Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni Haji uzinduzi huo utafanyika kituo cha Afya Chumbuni Mjini Zanzibar.
Mdhibiti magonjwa - Kitengo cha Chanjo Wizara ya Afya Bw. Abdulhamid Ame akitoa ufafanuzi kuhusu Chanjo wakati wa Mkuta na wandishi wa Habari.
Muandishi wa Habari wa Staa TV Abdallah Pandu akitaka ukiuliza swali kuhusu wiki ya Chanjo Afrika.

Baadhi ya wandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mratibu wa Chanjo Zanzibar Bw. Yusuf Haji (hayupo pichani) kuhusu siku ya Chanjo Afrika katika ukumbi wa Mazsons Hotel Shangani Mjini Zanzibar.PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR.
Na Salum Vuai, MAELEZO

WAKATI bara la Afrika linaanza wiki ya chanjo za kujikinga na maradhi kwa watoto kesho (April 24), Waziri wa Afya Mhe. Juma Duni Haji, anatarajiwa kuzindua wiki hiyo kwa upande wa Zanzibar.

Uzinduzi huo ambao unafanyika Tanznaia nzima na katika nchi zote za bara la Afrika, kwa Zanzibar umepangwa kufanyika kitaifa katika kituo cha afya Chumbuni Wilaya ya Mjini.

Aidha shughuli kama hiyo itafanyika katika wilaya zote kumi za Unguja na Pemba, ambapo wakuu wa kila wilaya wanatarajiwa kuzindua katika ngazi vituo mbalimbali vilivyomo katika wilaya zao, kuanzia leo Aprili 24 hadi 30, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Mazson iliyoko Shangani mjini Unguja, mratibu wa chanjo Zanzibar Yussuf Haji Makame, alisema huduma hizo zinatolewa kutokana na agizo la Shirika la Afya Ulimwenguni (W.H.O), kwamba ifikapo wiki ya mwisho ya mwezi Aprili kila mwaka, nchi zote za bara la Afrika zitoe huduma hizo kitaifa.

Alifahamisha kuwa, zoezi hilo linawalenga watoto wote walio chini ya miaka miwili ambao, ama hawakukamilisha chanjo au hawajapata kabisa katika awamu iliyopita.Aidha, alisema dhamira ya chanjo hizo ni kuwakinga watoto na maradhi mbalimbali yanayoweza kuzuilika kwa chanjo ikiwemo polio, pepo punda surua na mengineyo.

Afisa huyo aliwataka wananchi wote wenye watoto wa umri huo na wengine walio chini ya miaka mitano, kuwapeleka watoto wao vituoni na kuhakikisha wanapata chanjo hiyo na kumaliza dozi ili kuwakinga na maradhi hayo, na hivyo kuliwezesha taifa kuwa na kizazi chenye afya bora.Alisema kazi hiyo itaanza katika vituo vyote mawilayani kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku zote saba. Akitoa takwimu za hali ya maradhi ya surua kwa mujibu wa utafiti wa W.H.O, Makame alisema mwaka 2011 vifo 158,000 vilivyosababishwa na ugonjwa wa surua viliripotiwa.

Alisema ripoti hiyo ilifafanua kuwa, kwa mujibu wa takwimu hizo, vifo 430 vilitokea kila siku, na kwamba kila baada ya saa moja kuliripotiwa vifo 18.Kwa upande wake, Afisa Mdhibiti Magonjwa katika kitengo cha chanjo Zanzibar Abdulhamid Ameir, alisema katika muongo wa chanjo barani Afrika ulioanza mwaka 2011 ambao unatarajiwa kukamilika 2020, mikakati madhubuti inahitajika kuhakikisha magonjwa yanawakumba watoto yanatoweka kabisa.

Miongoni mwa mikakati hiyo, ni kutoa dozi ya pili kwa chanjo ya kukinga surua kuanzia mwezi ujao, tafauti na miaka iliyopita ambapo kulikuwa kukitolewa dozi moja tu.Alisisitiza kuwa, lengo la W.H.O. ni kuona ifikapo mwaka 2020 tatizo la maradhi ya watoto yanamalizwa au kupunguzwa kwa asilimia kubwa.Alihitimisha kwa kusema, huduma zinazozinduliwa leo, zinafanyika Tanzania nzima, na akasisitiza wananchi wasipuuze kuwapeleka watoto wao ili kuwakinga na maradhi hayo.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa