Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » DIDA ASHIKILIA NAMBA YA KASEJA

DIDA ASHIKILIA NAMBA YA KASEJA


Kwa sasa Yanga ina makipa watatu ambao ni Dida, Juma Kaseja na Mustafa Ali ‘Barthez’. Dida ndiye kipa nambari moja wa Taifa Stars.

KOCHA wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali, amesema kuwa kipa nambari moja wa Yanga atajulikana wiki moja baada ya kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ kurejea mazoezini akitokea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.
Pondamali alisema: “Tutaamua kipa namba moja baada ya Dida kufanya mazoezi na Yanga kwa takribani wiki moja. Hatuwezi kusema yeye ni kipa namba moja wakati hatujampima. Pengine kuwepo kwake kwenye timu ya taifa kuna mawili, anaweza kuwa amepanda kiwango au pia ameshuka.
“Timu ya taifa kuna mbinu tofauti na hizi tunazowapa hapa Yanga, falsafa za makocha nazo ni tofauti na ndiyo maana unaona pia Kocha Msaidizi (Leonardo Neiva) amekuwa akitoa vitu vipya kwa makipa wetu, hii itamfanya Dida aje kupimwa na mazoezi mapya ili kuamua nani ni namba moja wa kikosi chetu.”
Kwa sasa Yanga ina makipa watatu ambao ni Dida, Juma Kaseja na Mustafa Ali ‘Barthez’. Dida ndiye kipa nambari moja wa Taifa Stars.
CREDIT:MWANASPOTI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa