Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kutotimia kwa akidi ya wabunge wa Rwanda kulisimamisha kwa
dakika 15 kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kilichoanza jana
jijini hapa.
Ikiwa ni kikao chake cha kwanza baada ya
kufunguliwa rasmi juzi, Bunge hilo lilikuwa na ajenda mbili, zote zikiwa
ni uwasilishaji wa ripoti za kamati za kilimo, utalii na maliasili
pamoja na ya usuluhishi wa migogoro.
“Naomba mwongozo wako Spika. Inakuwaje tunaendelea
na kikao ambacho kitapitisha hoja hii wakati akidi ya wabunge kutoka
Rwanda haijatimia?” alihoji Nusra Omar kutoka Uganda.
Spika Margaret Zziwa alilazimika kuita majina ya
wajumbe wote wa Bunge hilo ili kujiridhisha. Alisema kutokana na kanuni
za Bunge hilo, alilazimika kulisitisha ili kutoa muda kwa wasiokuwepo
kama hawako mbali waingie ukumbini.
Kutokana na hilo, Zziwa alitoa mwongozo kuwa
“Kanuni Namba 13 ya Mwenendo wa Eala inasema ili kikao cha Bunge
kiendelee, lazima kuwe na nusu ya wabunge waliochaguliwa ambao
watajumuisha wajumbe watatu kutoka katika kila nchi wanachama. Hivyo
naliahirisha Bunge hili kwa dakika 15”.
Bunge hilo linafanyika jijini hapa kwa mara ya
kwanza tangu utaratibu wa kufanya vikao vyake katika miji tofauti ya
nchi wanachama upitishwe. Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wamedai kuwa
hiyo ni njama ya Rwanda kutotaka vikao hivyo vifanikiwe.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment