Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » HATIMAYE WAKAZI MABWEPANDE WAKUBALI MAENEO YAO KUPIMWA

HATIMAYE WAKAZI MABWEPANDE WAKUBALI MAENEO YAO KUPIMWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Prof. Anna Tibaijuka.
Hatimaye  wananchi wa Mabwepande ambao awali walitaka kugomea zoezi la utambuzi na upimwaji wa maeneo yao, wamelikubali baada ya kuelezwa kwa kina faida zake.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabwepande, Abdallah Kunja, alisema zoezi hilo linalofanywa na Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, lilitaka kuingia dosari kutokana na baadhi ya wananchi kutaka kuligomea kwa kuhofia maeneo yao kuchukuliwa kijanja.

Alisema baada ya hali hiyo kujitokeza, waliitisha mkutano wa wananchi uliohudhuriwa pia na maofisa wa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni.

Kunja alisema maofisa hao wa ardhi walitumia mkutano huo kuwaelewesha wananchi faida za zoezi hilo na pia wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi.

“Sisi kama viongozi wa serikali ya mtaa tunashukuru zoezi hilo kutokwama, kwani ni kwa maendeleo ya wananchi wetu kutokana na kwamba, ardhi ikishapimwa thamani yake inapanda,” alisema Kunja.

Alisema zoezi tayari limenza na linaendelea vizuri na hakuna malalamiko ya mwananchi yoyote kama ilivyokuwa imejitokeza awali.

Kunja alisema kutokana na wananchi kulielewa vizuri zoezi hilo hata wale, ambao walikuwa hawaguswi nalo wamewasilisha maombi yao wakitaka nao waingizwe kwenye mradi huo.

“Kutokana na maombi hayo ya wananchi hao, tunaiomba manispaa isikilize maombi hayo na kuyafanyia kazi ili wananchi wote wa Mabwepande wapimiwe maeneo yao kwa maendeleo ya mtaa wetu na wananchi wake,” alisema Kunja.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa