Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila
amewasilisha mahakamani pingamizi la awali dhidi ya kesi ya
aliyofunguliwa na kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL),
katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
IPTL kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African
Power Solutions (T) Limited na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hizo,
Harbinder Sigh Seth imemfungilia Kafulila kesi ya kashfa.
Katika kesi hiyo, walalamikaji kwa pamoja
wanaiomba mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe fidia ya Sh310 bilioni
kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia fedha
kutoka katika Akaunti ya Escrow, kwa njia zisizo halali.
Pia walalamikaji hao wamewasilisha mahakamani hapo
maombi kutaka mahakama hiyo imzuie Kafulila kuendelea kuzungumzia jambo
lolote kuhusu walalamikaji hao, hadi kesi ya msingi itakapoamuriwa.
Hata hivyo, Kafulila ambaye katika kesi hiyo
anatetewa na Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na
Mtandao wa Walinzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu, amewasilisha
pingamizi la awali dhidi ya kesi hiyo.
Katika pingamizi hilo, anadai kuwa mlalamikaji wa
kwanza, IPTL hana haki ya kisheria ya kumfungulia kesi kwani kama
inadaiwa kuwa iliuzwa kwa PAP, basi haipo na hivyo haina uhalali wa
kushtaki.
Katika hoja nyingine, anadai kuwa hati ya kiapo
cha mlalamikaji wa tatu (Seth) ina dosari za kisheria kwa kuwa wakili
aliyesaini kiapo hicho anadai kuwa alikuwa akimfahamu Seth na wakati
huohuo anadai kuwa Seth alitambulishwa kwake na mtu mwingine.
Anadai pia kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment