Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ukubwa wa familia unachangia zaidi umaskini nchini, Benki ya Dunia (WB) imeeleza.
Kwa mujibu wa ripoti ya benki hiyo, mambo mengine
yanayochangia umasikini kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kiwango cha elimu,
miundombinu, ajira na kuhama makazi.
“Familia zenye watoto zaidi ya kumi kwa mwaka
2012, ni masikini kwa asilimia 45. Kiwango hicho kimeongezeka kutoka
asilimia 42 kwa mwaka 2007. Kiwango cha umasikini kwa familia zenye
watoto chini ya watatu ni chini ya asilimia 20,” inaeleza ripoti hiyo.
Akizungumzia ripoti hiyo, Dk Adolf Mkenda, kaimu
katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, alisema: “Ni kweli familia zenye watoto
wengi zinashindwa kutimiza mahitaji yote ya msingi. Wazazi wanaelemewa
katika matibabu, ada, chakula na wakati mwingine malazi.”
Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS), Dk Albina Chuwa alisema: “Njia pekee ya kuondokana na umaskini
katika familia yenye watoto wengi ni kuongeza uwekezaji ili kukidhi
mahitaji ya kila mwanafamilia kama walivyofanya India.”
Ukiacha ukubwa wa familia, kiwango cha elimu kinashika nafasi ya pili kwa kuchangia umaskini.
Ajira zenye mshahara zimeelezwa kupunguza umaskini.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa watumishi wa Serikali
ndio wanaoongoza katika kupunguza kiwango cha umaskini kutokana na
kunufaika na mishahara.
Inaeleza kuwa kiwango cha umaskini kwa watumishi
wa Serikali ni asilimia 7 wakati waliojiajiri wamepunguza kiwango cha
umaskini kwa asilimia 32.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment