Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » LHRC:VITENDO VYA UKATILI MAJUMBANI VYAKITHRI NCHINI

LHRC:VITENDO VYA UKATILI MAJUMBANI VYAKITHRI NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
 
Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zinaonyesha kuwa vitendo vya ukatili wa majumbani pamoja na ubakaji vimekithiri nchini kati ya Januari na Juni, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe, alisema katika kipindi hicho, wanawake pamoja na wasichana 2,878 walibakwa na vitendo 3,633 vya ukatili dhidi yao viliripotiwa kwenye vituo vya polisi nchi nzima.

Alisema kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi, idadi ya watu wanaishi vijijini, lakini bado huduma za jamii, kama vile upatikanaji wa maji, huduma za afya, shule pamoja na umeme vijijini ni duni.

“Takwimu zinaonyesha kuwa bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana na gharama kubwa za saruji na vifaa vya ujenzi. Kwa mfano, katika suala la upatikanaji wa maji, makazi 3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo salama, ukilinganisha na makazi 1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi nzima,” alisema.

Alisema idadi ya wananchi 11,359,090 wanategemea kilimo kama shughuli kuu ya uchumi na kwamba, wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono na kwamba, uwekezaji katika mashamba makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa. Mlowe alisema pia kiwango cha elimu bado kipo chini nchini, kwani kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi, idadi ya Watanzania waliopata elimu rasmi ni 14,495,447, kati yao 11,848323 wamehitimu elimu ya msingi, huku wenye elimu ya chuo kikuu wakiwa 337.881 tu.

Utafiti huo umeonyesha kumekuwapo na ongezeko la tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi, mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na watu wenye ulemavu wa ngozi kutokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya haki za binadamu, pia kukosekana kwa elimu ya haki za binadamu katika mifumo ya elimu.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa