Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Migogoro ya kisiasa katika nchi nyingi za Afrika ni miongoni mwa
sababu inayokwamisha uwekezaji kutoka nje na jitihada za kupambana na
umaskini na ukuzaji wa uchumi wa mataifa hayo.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika jijini hapa jana, makamu wa rais wa Taasisi ya
Kudhamini Uwekezaji (Miga), Michael Wormser alisema machafuko ya kisiasa
yanafanya wawekezaji wengi kuogopa kufanya hivyo barani Afrika.
“Hatari ambazo zinawapa wasiwasi wawekezaji na
wakopeshaji mara nyingi zinahusiana na imani ndogo katika mifumo ya
mahakama na taasisi za udhibiti, utawala mbovu, rushwa na uhaba wa
utawala wa sheria,” alisema.
“Kinachotokea hivi sasa katika nchi nyingi ni
kutokuwapo kwa usimamizi wa mikataba, machafuko ya kisiasa na kuyumba
kwa uchumi mkuu wa nchi husika.”
Alisema nchi nyingi za barani Afrika zinakabiliwa
na uwekezano mkubwa wa kupoteza mitaji ambayo ni muhimu katika ukuzaji
wa uchumi. Alisema Tanzania ina usalama na fursa nyingi za uwekezaji
zikitumiwa vizuri
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment