Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » NAIBU SPIKA NDUGAI: NITAACHIA UBUNGE 2020

NAIBU SPIKA NDUGAI: NITAACHIA UBUNGE 2020

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mbunge wa Kongwa, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai
 
Mbunge wa Kongwa, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, amesema atagombea tena ubunge katika jimbo hilo kwa mara ya mwisho Mwaka 2020.
 
Ndugai aliliambia NIPASHE jana kuwa  kwa miaka 15 aliyotumikia jimbo hilo kama mbunge, amefanikisha kupatikana kwa maendeleo na kwamba anaamini wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hatakabiliwa na ushindani wa aina yoyote.
 
“Nina hakika mwakani hakuna atakayechukua fomu hapa, lakini nikimaliza awamu ijayo, sitagombea tena,” alieleza Ndugai huku akionyesha kujiamini.
 
Alipotakiwa kueleza ikiwa nia yake ya kutogombea tena iwapo atapata na kumaliza kutumikia kipindi hicho, inatokana na mabadiliko ya Katiba ambayo mchakato wake unaendelea, Ndugai alisema hiyo siyo sababu.
 
Alisema miaka 20 na itatosha kuwaachia wengine wenye uwezo na nia ya kutumikia umma.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa