Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UDA YALALAMIKIWA KUNYASANYASA ABIRIA

UDA YALALAMIKIWA KUNYASANYASA ABIRIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra)
Chama Cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua) kimelalamikia huduma za usafiri wa mabasi Uda kwa kuwanyanyasa abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chakua, Hassan Mchanjama, akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni alisema Uda wamesaidia kupunguza tatizo la usafiri kwa wakazi wa jiji, lakini yamekuwa ni kero na usumbufu kwa abiria.

Alisema wamekuwa wakipokea malalamiko ya abiria wakiyashutumu mabasi hayo kwa kukatisha ruti na kupakia abiria zaidi ya mara mbili kwa ruti moja.

“Uda pamoja na kupunguza tatizo la usafiri japo hayajakidhi mahitaji ya abiria, yamekuwa ni kero kubwa. Kwani yanapakia ruti moja zaidi ya mara mbili. Hili ni tatizo. Badala ya kumsaidia abiria linamuongezea abiria usumbufu wa kushuka na kupanda wakati safari ni moja,” alisema Mchanjama.

Alisema pamoja na kulalamika mara kwa mara kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra), bado hakuna juhudi za kupungua kwa tatizo hilo.

“Tunaitaka Sumatra watumie mamlaka yao kuyadhibiti mabasi haya, ambayo yameonekana kuwa kama Sumatra imeshindwa kuyadhibiti. Haiwezekani magari yakakatisha rudi bado yanaachiwa. Abiria wananyanyaswa bila ya sheria yoyote kuchukuliwa dhidi yao. Kama Sumatra imeshindwa kuwadhibiti ina maana wameshindwa kazi iachwe ngazi,” alisema.

Msemaji wa Uda, George Maziku, akizungumzia suala hilo alisema: “Shirika letu linaruhusiwa kweda ruti zaidi ya 10. Kwa hiyo, wanaolalamika hawajui utaratibu wa kusafirisha abiria” alisema Maziku.

Naye Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray, alisema wanatambua kuwapo kwa changamoto hizo na hivi karibuni wamekamata mabasi 25 ya Uda kwa makosa hayo.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa