Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Saed Kubenea
Kwa mujibu wa taarifa ya Kibatala, anakata rufaa kupinga sehemu ya uamuzi wa Mahakama Kuu katika kipengele kinachoeleza kwamba pamoja na kwamba Bunge Maalum la Katiba lina mipaka na linatakiwa kutekeleza mamlaka yake kupitia Rasimu na kifungu cha 9 (2).
Sababu nyingine ya kukata rufaa ni kwamba baada ya kusema Bunge Maalum la Katiba linaweza kurekebisha na kuboresha Rasimu, Mahakama ilitakiwa kusema kwamba marekebisho na maboresho ni tofauti na kutoa kabisa vifungu kadhaa kuwa suala la uwazi.
“Tutawasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama ya Rufani wakati tukisubiri Oktoba 7, mwaka huu kusomewa hukumu ya jumla ya maombi ya kuhoji uhalali na mamlaka ya Bunge hilo,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Kibatala kupitia taarifa yake alisema ataangalia pia uwezekano wa kufungua shauri chini ya hati ya dharura katika eneo fulani la mchakato na kwamba ni muhimu kuishirikisha Mahakama.
Aidha, aliishukuru Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa kile ilichofanya kwa uwezo wake, na imechangia sana maendeleo ya sheria na ya mchakato mzima, lakini bado kuna kiu katika maeneo waliyoiainisha na wanaona rufaa ni muhimu.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment