Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » BENKI YA NMB YAWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA NA USHINDE‏

BENKI YA NMB YAWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA NA USHINDE‏




 Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB, Salie Mray (kulia), akimkabidhi Florence Kasenene cheti cha ushiriki katika  promosheni ya Weka na Ushinde katika hafla iliyofanyika viwanja vya benki hiyo Tawi la Sinza Mori Dar esaSalaam leo asubuhi. Kasenene alijishia bajaj.

 Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB, Salie Mray (kulia), akimkabidhi Florence Kasenene, akimkabidhi funguo wa bajaj, Florence Kasenene katika hafla hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Ofisa Habari wa benki hiyo, Doris (kushoto), akizungumza kwenye sherehe hiyo.
 Mshindi wa pikipiki, Mariam Mburinyingi  akifurahi kushinda pikipiki hiyo na mmoja wa maofisa wa benki hiyo.
 Mshindi wa baiskeli, akiijaribu  kuiendesha baada 
ya kukabidhiwa.
 Washindi wa baiskeli wakiwa na baiskeli zao pamoja 
na maofisa wa benki hiyo.
 Baiskeli walizokabidhiwa washindi.
 Pikipiki walizokabidhiwa washindi hao.
Bajaj na pikipiki zilizokabidhiwa kwa washindi.

Dotto Mwaibale

BENKI ya NMB imetoa zawadi za pikipiki, bajaj na baiskeli kwa  washindi wa promosheni ya Weka na Ushinde inayoendeshwa na benki hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB, BENKI YA NMB YAWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA NA USHINDI Salie Mray alisema washindi waliopata zawadi kwa mwezi wa kwanza wa promosheni hiyo  ni wa Kanda ya Dar es Salaam.

"Kwa Kanda ya Dar es Salaam tuna washindi 30 ambao zawadi zao tunawakabidhi leo 'jana' na wale wa Kanda zingine watapewa zawadi zao kwenye kanda zao" alisema Mray.

Aliwataja washindi walioshinda bajaj ni watano, washindi watatu wameshinda pikipiki za magurudumu mawili na washindi 22 wamejishindia baiskeli aina ya Phoenix.

Alisema katika promosheni hiyo kuna zawadi nyingi za kushindania zenye thamani ya sh.milioni 500 hivyo watanzania wachangamkie fursa hiyo kwani droo zingine zitaendelea kuchezeshwa kila Jumatatu.

Alisema zawadi zilizotolewa jana zinatokana na droo ya nne iliyofanyika kwa nchi nzima ambapo tayari wamepatikana washindi wa 17 wa bajaj, 16 pikipiki na 132 baiskeli aina ya Phoenix.

Mray alisema hiyo ni fursa kwa wateja wao kwani kila mtu anaweza kushinda ili mradi tu afuate taratibu za kushiriki ambazo ni kuweka fedha kwenye akaunti yake mara nyingi awezavyo ili kujiongezea naafasi zaidi kushinda. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa