Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » BOT KUFANYIA KAZI NOTI YA SH1,000

BOT KUFANYIA KAZI NOTI YA SH1,000

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
. Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema imeanza kufanyia kazi malalamiko ya kukosewa kwa picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere.
Mkurugenzi wa huduma za kibenki wa BoT,Emmanuel Boaz aliwaambia waandishi wahabari mjini hapa kuwa tayari benki hiyo imeanza kuzifanyia kazi tuhuma hizo baada ya kusoma katika mitandao ya jamii.
Boaz alisema hayo baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kuhusu malalamiko iliyopokea na hatua zilizochukuliwa ili kubadili noti hiyo.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo alisema BoT haijapata taarifa rasmi kutoka kwa mtu yoyote, lakini wameamua kuzifanyia kazi taarifa hizo. “Na sisi tumesoma katika mitandao. Hakuna taarifa rasmi tuliyoipata, lakini hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo tutachukua hatua za kubadili haraka,” alisisitiza Boaz.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, suala la picha kukosewa sio geni kwani ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa marais wastaafu na BoT ililazimika kubadili haraka ili kutoharibu mtazamo wa Taifa.
Alitoa mfano wa picha ya Mwalimu Nyerere kukosewa na kuonekana nguo aliyovaa imefanana na blauzi lakini pia picha ya Rais Ally Hassani Mwinyi ambayo ilionekana shingoni ana mikunjo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa endapo itabainika kama noti hizo zina kasoro, zitarekebishwa.
Hivi karibuni, mitandao ya kijamii iliwakariri wanafamilia ya Rais huyo wa kwanza wakilalamikia picha hiyo kwenye noti ya Sh1,000, wakidai kuwa imekosewa.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa