Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KIWANGO CHA UMASKINI CHASHUKA NCHINI

KIWANGO CHA UMASKINI CHASHUKA NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Kiwango cha umaskini nchini kimepungua kutoka asilimia 34.4 hadi asilimia 28.2 huku asilimia 96 ya  Watanzania wakiwamo wakulima wakiendelea kutumia zana duni za kilimo kama jembe la mkono.

Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, wakati wa uzinduzi wa chapisho kuu la utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi wa mwaka 2011/12 kwa upande wa Tanzania Bara.

Baadhi ya taarifa muhimu zilizopo kwenye chapisho hilo ni pamoja na zile zinazohusu mapato, matumizi na manunuzi ya kaya, elimu, afya, shughuli za kiuchumi na ajira.
Mkuya alisema utafiti huo ni wa nne kufanyika nchini tangu uhuru mwaka 1961 ambao unaonyesha mwenendo wa hali ya umaskini kwa kuangalia kiwango chake na makundi yaliyoathirika zaidi. 

Waziri Mkuya, alisema matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kwamba umaskini nchini umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2011/12.

Alisema matokeo hayo pia yanaonyesha kwamba kiasi cha Sh. 36, 482 kinahitajika kukidhi mahitaji ya msingi ya mtu mzima kwa mwezi ikilinganishwa na Sh. 19, 201 kwa mahitaji ya jinsi hiyo mwaka 2007.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa kiasi cha Sh. 26, 085 kinahitajika kukidhi mahitaji ya chakula kwa mtu mzima kwa mwezi ikilinganishwa na Sh. 12, 444 kwa mahitaji kama hayo mwaka 2007.

“Hii ni hatua nzuri inayostahili kuendelezwa kwa kuongeza juhudi zaidi katika eneo la ukuaji wa uchumi ili kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii yetu,” alisema.

Hata hivyo, utafiti huo unaonyesha kwamba asilimia 96.5 ya kaya zinazojishughulisha na kilimo bado zinatumia jembe la mkono huku asilimia 0.1 pekee ya kaya ndiyo zinazotumia zana za kisasa kama vile jembe la plau na trekta.

Aidha, ushiriki wa benki katika shughuli za biashara ngazi ya kaya pia bado ni mdogo katika utoaji wa mitaji ya kuanzisha biashara katika ngazi hiyo.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu, alizishauri taasisi za kifedha zikiwamo benki kupunguza kiasi cha riba kwa wananchi wanaotaka kukopa fedha kwenye
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa