Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KURA YA MAONI MKOROGANO

KURA YA MAONI MKOROGANO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais Jakaya Kikwete 
tatu tofauti ndani ya wiki moja kuhusu tarehe ya Kura ya Maoni kupitisha KatibaInayopendekezwa, kimeelezwa na watu wa kada mbalimbali nchini kuwa ni matokeo ya viongozi wa Serikali kukosa uongozi wa pamoja.
Wakizungumza na Mwananchi Jumamosi, wasomi, wanaharakati, viongozi wa dini na wanasiasa wamesema kauli hizo zinawachanganya Watanzania, kwamba mpaka sasa hakuna anayejua tarahe rasmi ya kufanyika Kura ya Maoni.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alilieleza gazeti hili kuwa  kura hiyo ingefanyika Machi 30 mwakani na kwamba upigaji kura utatanguliwa na kampeni ambazo zitafanyika kwa siku 30, kuanzia mwanzoni mwa Machi ili kushawishi Katiba Inayopendekezwa iungwe mkono au kinyume chake kwa makundi yanayoipinga.
Siku moja baadaye, Rais Kikwete alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China alisema endapo mipango yote itakwenda kama inavyoandaliwa, Watanzania wataipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa Aprili mwakani.
Kauli ya Jaji Werema pia ilipingwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva na kufafanua kuwa kura ya maoni haiwezi kufanyika Machi 30 mwakani kwa sababu kazi ya uandikishaji wa Daftari la Wapigakura haitakuwa imekamilika.
Utata umezidi kuongezeka baada ya jana katika mkutano wake na waandishi wa habari, Jaji Lubuva kusema kuwa Daftari la Kudumu la Wapigakura litakamilika Aprili 18 mwakani, huku taratibu zikieleza kwamba kura ya maoni itafanyika baada ya elimu kutolewa kwa wananchi na hutolewa kati ya miezi mitatu hadi sita.
Awali Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwahi kukaririwa akisema kuwa Kura ya Maoni ifanyike kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015, huku Rais Kikwete akikubaliana na viongozi wa vyama vya siasa kuwa kura ya maoni itafanyika baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti Mwalimu wa Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Faraja Christoms alisema, “Hayo ni matokeo ya kukosekana kwa uwajibikaji wa pamoja. Sina hakika kama AG ndiye alipaswa kutaja tarehe ya kura ya maoni, yeye ni mshauri tu.”
Alisema kitendo cha kauli ya AG kutofautiana na iliyotolewa na rais ambaye amemteua ni ishara mbaya katika utendaji kazi wa Serikali.
“Wakati mwingine kauli kama hizi zinaweza kuwavunja moyo walioteuliwa. Nakumbuka Waziri Mkuu Pinda aliwahi kutoa kauli ya kupinga maelezo ya Waziri wa Ujenzi, Magufuli (John). Tafsiri ya kilichotokea ni kukosekana kwa uwajibikaji wa pamoja,” alisema.
Naye Katibu Mkuu  wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita alisema kazi iliyobaki ni kuwahamasisha wananchi wakati wa kupiga kura ya maoni utakapofika  kwa maelezo kuwa kila mtu atapiga kura kutokana na anachokiamini.
Dk Mtaita alisisitiza pia kuboreshwa kwa Daftari la Wapigakura, akisema kuwa hilo ndilo litakuwa jambo la msingi ili kuwafanya Watanzania wote wenye sifa waweze kupiga kura, huku akiiomba Serikali kuhakikisha inasambaza nakala za kutosha za Katiba Inayopendekezwa.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa