Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SHAHIDI AELEZA KAMPUNI ILIVYOPATA USAJILI KESI YA MHANDO WA TANESCO

SHAHIDI AELEZA KAMPUNI ILIVYOPATA USAJILI KESI YA MHANDO WA TANESCO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Shahidi Atanas Kalihamwe, amedai mahakamani kuwa Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd ilipata zabuni katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) miezi minne baada ya kupata usajili.


Kadhalika, shahidi amedai katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando, mke wake Eva Mhando, na wenzao watatu, ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kujipatia Sh. milioni 31.7 kwa njia ya udanganyifu kwamba kabla ya hapo kampuni hiyo ilikuwa ikifanya shughuli zake bila usajili.

Kalihamwe ambaye ni Mkuu wa Manunuzi wa Tanesco, alitoa madai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi FrankMoshi anayesikiliza kesi hiyo wakati akiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai.

Alidai kuwa nyaraka za zabuni za kampuni ya SantaClara Supplies Ltd zinaonyesha zilisainiwa na Eva Steven William Agosti 5, mwaka 2011.

“Mheshimiwa hakimu kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd ilipata zabuni miezi minne baada ya  kusajiliwa kisheria na kwamba kabla ya hapo kampuni hiyo ilikuwa ikifanya shughuli zake ikiwa haina usajili,” alidai shahidi huko.

Hata hivyo, alidai kuwa kumbukumbu zinaonyesha tangu kampuni hiyo ishinde zabuni haijawahi kupata dosari kwa sababu ilitimiza majukumu yake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 18, mwaka huu itaakapotajwa na itaendelea kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri Desemba 8 hadi 10, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, Mhando anakabiliwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd, huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa