Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAZIRI WA FEDHA -SAADA MKUYA AONGOZA UZINDUZI WA CHAPISHO KUU LA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI 2011-2012-TANZANIA BARA

WAZIRI WA FEDHA -SAADA MKUYA AONGOZA UZINDUZI WA CHAPISHO KUU LA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI 2011-2012-TANZANIA BARA


 Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi akihutubia.
 Mwakilishi wa Benki ya Dunia,  Philippe Dongier, 
akihutubia katika hafla hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Ofisa kutoka Shirika la Maendeleo la DPG, Sinikka Antila, 
akitoa hutuba fupi kwa wageni waalikwa.
 Meneja wa Mazingira na Uchambuzi wa Takwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (TBS), Sango Abas Simba, akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa kuhusu chapisho hilo.
 Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto), akionesha kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Ofisa kutoka Shirika la Maendeleo la DPG, Sinikka Antila, Mwakilishi wa Benki ya Dunia,  Philippe Dongier na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (Dk. Albina Chuwa (kushoto), akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Beno Ndulu wakati wa uzinduzi wa chapisho hilo.
 Wadau wa masuala ya takwimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Maofisa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakiwa 
kwenye uzinduzi huo.
 Wanafunzi wa Chuo cha Takwimu nao walijumuika kwenye uzinduzi wa chapisho hilo.
  Wanafunzi wa Chuo cha Takwimu. 

Viongozi meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha Takwimu.

Dotto Mwaibale

TAKWIMU mbalimba za nchi zimetakiwa kutolewa na chombo chenye dhamana badala ya kutolewa kiholela jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya wakati akizindua Chapisho la Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/20012.

"Ni muhimu tafiti mbalimbali za maendeleo ya nchi zikatolewa na chombo chenye dhamana kwani kutolewa tofauti na chombo hicho zinaweza kuhatarisha maendeleo ya nchi" alisema Mkuya.

Katika hatua nyingine Mkuya alisema hali ya umaskini imeonekana kupungua nchini kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 kwa mwaka 2011/2012.

Alisema chapisho hilo huwa linaisaidia Serikali katika kutathimini na kurekebisha baadhi ya sera na mipango ya maendeleo ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa nchi.

"Wakati nazindua chapisho hili inaonyesha kwamba kiasi cha sh. za Tanzania 36,482 kinahitajika katika kukidhi mahitaji ya msingi ya mtu mzima mmoja kwa mwezi ukilinganisha na kiasi cha cha sh. 19,201 kwa mahitaji ya aina hiyo ya mwaka 2007.

Alisema katika maeneo ya vijijini kiwango cha umaskini kimeonekana kupungua lakini hali hiyo imekuwa ni changamoto kwani asilimia kubwa ya watu wa vijijini wanatumia  zana za kilimo za zamani.

"Utafiti unaonyesha kuwa kila watu 100 walikuwa na uwezo wa kufanya kazi mwaka 20011/12 watu 75 walijishighulisha na kilimo na uvuvi hata hivyo matumizi ya duni ya zana za kilimo bado imekuwa ni changamoto kubwa inayoedelea kutukabili,"alisema.

"Utafiti unaonyesha kwamba asilimia 96.5 ya kaya zinazojishughulisha na kilimo bado zinatumia jembe la mikono na asilimia 0.1 tu ndiyo zinatumia zana za kisasa za kilimo likiwemo jembe na plau na trekta.

Aliongeza kuwa watu wengi hawana ushiriki wa benki katika shughuli za kibiashara wa ngazi ya kaya bado ni mdogo katika utoaji wa mitaji ya kuanzisha biashara katika ngazi hizo.


Alisema ni muda wa Serikali sasa kuweza kuwafahamisha hata kwa kuwapa wananchi njia za kujiari wenyewe ili kuweza kupunguza kabisa hali ya umaskini nchini. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa