Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » CHEKA ATAMBA KUMCHAPA SHAURI KWA KO

CHEKA ATAMBA KUMCHAPA SHAURI KWA KO

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Cosmac Cheka ametamba kumchapa mpinzani wake kwa KO katika pambano lisilokuwa la ubingwa.

Cheka atazichapa na Ramadhani Shauri siku ya Mwaka mpya katika pambano la kuuaga mwaka.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Cheka alisema kuwa amejipanga vyema kuhakikisha anashinda pambano hilo.

Alisema licha ya ugumu alionao mpinzani wake lakini atapigana kuhakikisha anatetea rekodi yake ya kutopigwa na bondia kutoka hapa nchini.

"Nimejiandaa vyema na nitahakikisha naendelea kushikiria rekodi yangu ya kutopigwa na bondia wa Tanzania, " alisema Cheka.

Alisema, katika pambano hilo akishindwa kumpiga mpinzani wake kwa KO basi atahakikisha atampiga kabla ya raundi ya tatu kumalizika.

Alisema kuwa kutokana na maelekezo aliyoyapata kwa mwalimu wake ni dhahiri kuwa atampiga mpinzani wake.

Chanzo;Mwananchi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa