Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TAMISEMI KUWAFUKUZA KAZI WAKURUGENZI WASIO WAJIBIKA

TAMISEMI KUWAFUKUZA KAZI WAKURUGENZI WASIO WAJIBIKA

Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI ) Jumanne Sagini amesema hatasita kuchukua hatua stahiki, ikiwemo kuwafukuza kazi baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji watakaobainika kushindwa kusimamia matumizi ya fedha za umma na miradi inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo.
Ametoa onyo hilo wakati akifunga mafunzo ya sheria mpya ya ununuzi wa umma yaliyowashirikisha wajumbe wa bodi za ununuzi, wanasheria na wakurugenzi wa halmashauri nane zinazotekeleza mradi wa uimarishaji wa miji 18 ya tanzania bara, yaliyofadhiliwa na benki ya Dunia kwa ushirikiano na taasisi ya kiufundi ya ubelgiji kwa lengo la kuzijengea uwezo halmashauri hizo katika kuandaa na kusimamia mifumo ya ununuzi kwa weledi na tija zaidi.

Katibu mkuu huyo ameongeza kuwa manunuzi yanatumia zaidi ya asilimia 70 hadi 80 ya bajeti za halmashauri, hivyo amewasisisitiza watendaji hao kuhakikisha wanasimamia kwa weledi wa kutosha katika eneo la manunuzi ili kuondoa malalamiko na kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa zikibainishwa katika taarifa ya kila mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

Aidha Sagini amedai kuwa kumekuwepo na tatizo la utumiaji wa fedha pasipo kufuata taratibu sahihi, ucheleweshaji wa maamuzi ya kufanya manunuzi kwa wakati kutokana na wataalam kutokuwa na uwezo wa kutosha katika ununuzi, utayarishaji wa nyaraka sahihi za ununuzi na uamuzi wa aina ya njia ya ununuzi, mambo ambayo amesema yanachangia katika utekelezaji mzuri wa kandarasi husika.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa