Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SERIKALI YAFUNGA VITUO VYA WATOTO YATIMA

SERIKALI YAFUNGA VITUO VYA WATOTO YATIMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imevifunga baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima katika maeneo mbalimbali nchini kwa kukiuka sheria ya uanzishwaji wake na wamiliki kujinufaisha binafsi.

Sambamba na hilo, pia imefuta kutoka kwenye orodha ya kutoa huduma ya kulea watoto yatima baadhi ya vituo vya aina hiyo vilivyo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, huku vile vya mkoani Iringa vikiendelea kufanyiwa uchunguzi.
Tangazo la kufungwa na kufutwa kwa vituo hivyo lilitolewa jana na Kaimu Kamishna Msaidizi Haki za Mtoto na Marekebisho ya Tabia wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Steven Gumbo, wakati wa semina ya kupanga mikakati ya malezi mbadala ya familia kwa mikoa yenye vituo vingi ya kulelea watoto yatima iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Gumbo alisema uamuzi wa kuvifunga na kuvifuta vituo hivyo umechukuliwa na serikali baada ya kufanya utafiti katika mikoa 25 na kubaini vipo zaidi ya 300, huku baadhi vikiwa vinaendeshwa bila leseni.
“Katika utafiti wetu wa mwaka 2011, tulibaini vituo vingi havina ubora na vilifunguliwa bila idhini ya Idara ya Ustawi wa Jamii. Mpango wa serikali kwa sasa ni kuvipunguza ili vibaki vichache vyenye ubora sasa kwa kushirikiana na asasi za kiraia kama SOS, tumeanza kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa malezi mbadala ili kuondoa udanganyifu kuwa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi lazima wakae kwenye vituo,” alisema Gumbo.
Akizungumza kuhusu uamuzi huo wa serikali, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Hai, Helga Saimon, alisema wilaya hiyo awali ilikuwa na vituo 22 vya kulelea watoto yatima, lakini baada ya uchunguzi, saba ndivyo vimekidhi vigezo vya kisheria.
“Kwa ujumla tulibaini mambo ya ajabu, kituo kimoja tulikuta mmiliki ni shoga na alikuwa akiwafanyisha watoto ushoga na baadhi ya vituo watoto wanabadilishwa majina kwa sababu zisizoeleweka. Hawa wote tumewafungulia kesi mahakamani,” alisema Helga.

Chanzo:MTanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa