Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » POLISI: MADEREVA WOTE WALIOSABABISHA AJALI KWA UZEMBE ZIKIWEMO ZA HIVI KARIBUNI WATAFUTIWA LESENI ZAO

POLISI: MADEREVA WOTE WALIOSABABISHA AJALI KWA UZEMBE ZIKIWEMO ZA HIVI KARIBUNI WATAFUTIWA LESENI ZAO


KIKOSI cha Usalama Barabarani nchini, kimesema madereva wote waliosababisha ajali kwa uzembe zikiwemo za hivi karibuni, watafutiwa leseni zao.

Kamanda wa kikosi hicho, Mohamed Mpinga, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari akisisitiza kuwa, ili kukabiliana na wimbi la ajali jeshi hilo limeazimia kufuta leseni za madereva hao.

Alisema ajali za hivi karibuni, zimesababishwa na uzembe wa madereva; hivyo ni lazima wafutiwe leseni na hawapaswi kufanya kazi ya udereva nchini na taarifa zao zitawekwa kwenye tovuti ili waajiri wengine wasiwachukue.

"Kuanzia sasa, mabasi yote yaendayo mikoani tutakuwa tunaangalia yametoka kituoni saa ngapi kwenye maeneo mbalimbali hadi linapomaliza safari yake...likiwa mbele ya muda hatua stahiki zitachukuliwa," alisema.

Kamanda Mpinga ametoa pole kwa wafiwa waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali za hivi karibuni.

CHANZO : GAZETI LA MWANANCHI


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa