Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SUMATRA KUTANGAZA VIWANGO VIPYA VYA NAULI ZA DALADALA NA MABASI YAENDAYO MIKOANI LEO.

SUMATRA KUTANGAZA VIWANGO VIPYA VYA NAULI ZA DALADALA NA MABASI YAENDAYO MIKOANI LEO.


MAMLAKA ya Udhibiti, Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), leo inatarajiwa kutangaza viwango vipya vya nauli za daladala na mabasi yaendayo mikoani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolifikia gazeti hili, imesema mamlaka hiyo itatangaza viwango hivyo ikiwa ni siku chache baada ya Waziri wa Uchukuzi, Bw. Samuel Sitta kuitaka  SUMATRA ihakikishe mchakato wa kukokotoa nauli hizo unakamilika haraka na kuutangazia umma.

Bw. Sitta aliitaka mamlaka hiyo kuhakikisha mchakato huo uwe umekamilika na kuutangazia umma ifikapo Aprili 3 kutokana na wadau wa usafiri huo nchini kulalamikia ongezeko la nauli.

Tangu kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na ndani ya nchi, kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa wadau wakiitaka Serikali itathmini upya viwango vya tozo katika huduma za usafiri wa nchi kavu, majini.

Sehemu kubwa ya maoni ya wadau yamejikita katika haja ya kuangalia upya viwango vya nauli za usafiri wa umma na majini wakisema gharama za uendeshaji kwa watoa huduma zimepungua kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta.

Lengo la wadau na wananchi ni kutaka wanufaike kutokana na punguzo la kushuka kwa bei za mafuta.
CHANZO: MWANANCHI
 

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa