Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TRA kutoa mafunzo ya ukusanyaji kodi wa washiriki 150

TRA kutoa mafunzo ya ukusanyaji kodi wa washiriki 150


 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akikata utepe kwenye boksi lililokuwa na Mtaala utakaotumia katika mafunzo hayo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya washiriki 150 waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade(wa sita kutoka Kulia) na Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi Prof. Isaya Jairo (ITA) (wa Tano kutoka kushoto) wakiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo baada ya kuyazindua leo Jijini Dar es Salaam. 

 Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.


 - Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwakaribisha wageni katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa waajiriwa wapya Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo hayo na kuwataka washiriki kushiriki kikamilifu kwenye kipindi cha mafunzo ili waweze kuwa na mbinu thabiti za ukusanyaji kodi kwa maslahi ya Taifa
 Naibu Mkurugenzi kitengo cha Rasilimali Watu Bw. Victor Kimaro akiwaeleza washiriki wa Mafunzo namna mchakato ulivyofanyika na kuwataka kuthibitisha ubora wao katika kipindi chote cha mafunzo
 
 - Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Rished BADE akiongea na washiriki wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi na kuwataka kufanya kazi kama watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kutumia fursa hiyo kujiimarisha kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi ya ukusanyaji kodi inayohitaji uadilifu na ueledi wa hali ya juu katika kuitekeleza, wakati wa hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa