Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MWANAMUZIKI MWANADADA MTANZANIA MWENYE ASILI YA ITALIA KUTUMBUIZA HOTELI YA MEDITERRANEO JUMAMOSI JIJINI DAR ES SALAAM

MWANAMUZIKI MWANADADA MTANZANIA MWENYE ASILI YA ITALIA KUTUMBUIZA HOTELI YA MEDITERRANEO JUMAMOSI JIJINI DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mwanamuziki Chantal Saroldi kutoka Italia.

 Mwanamuziki Chantal Saroldi (kushoto), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Balozi wa Italia nchini, toka Italia.

 Balozi wa Italia nchini, Luigi Sccoto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, kuhusu tamasha la muziki litakalofanyika kesho Hoteli ya Mediterraneo iliyopo Kawe ambapo mwanamuziki huyo atatoa burudani.
Mkurugenzi wa Hoteli ya Mediterraneo waandaaji wa tamasha hilo, Samantar Abdinur Lusuf (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni  mwanamuziki Chantal Saroldi  na Mmoja wa Wakurugenzi wa Hoteli hiyo, Alas Abdinur.
 Balozi wa Italia nchini, Luigi Sccoto (wa pili kulia), akiwa meza kuu na mwanamuziki huyo. Kulia ni mpiga kinanda wa mwanamuziki huyo Gianluca Tagliazucchi na wakurugenzi wa hoteli hiyo waandaaji wa tamasha hilo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Dotto Mwaibale

Mwanamuziki wa miondoko ya Jazz kutoka  nchini Italia Mwenye asili ya Tanzania Chantal Saroldi anataraji kutumbuiza  katika Hafla maalumu ya kusherehekea Siku ya Taifa la Italia ambapo raia wa Italia waishio nchini  watajumuika pamoja kwenye viunga vya ubalozi wa Italia ili kusherehekea Siku hiyo.

Mwanamuziki  Chantal Saroldi  mwenye asili ya Italia na Tanzania  alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea kabila la Wachaga.

Chanty yupo nchini kwa ajili ya ziara maalumu ya Muziki ambapo  kesho anatarajia kutumbuiza katika hoteli ya Mediterraneo ya jijini Dar esalaam na Juni 2 anataraji kutumbuiza katika  hafla maalumu inayoandaliwa na ubalozi wa Italia nchini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Taifa hilo.

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Scotto,  alisema kuwa katika kuzingatia kuwa mwanadada Chantal ni mwanamuziki mahiri waratibu wa sherehe hizo wamemchaguliwa kuja kutumbuiza katika hafla hiyo kwa kuwa ni nembo muhimu inayoziunganisha nchi mbili hizi za Tanzania na Italia.

Katika hatua nyingine mwanadada huyo alisema kuwa anajilaumu kwa kutojifunza lugha ya mama yake ambayo ni kiswahili, huku akibainisha kuwa mikakati ni  kujifunza lugha ya Kiswahili.

Mwanamuziki huyo amewahi kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya dhahabu katika kipengele cha uhariri na uandishi wa nyimbo ikitolewa na Disc Festival. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa