Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Poul Makonda akiongea na umati wa madereva na
wapiga debe waliofurika ndani ya kituo cha mabasi Ubungo mapema leo
ambapo amewataka madereva kuacha mgomo na waendelee na safari huku
matatizo yao ya msingi yakishughulikiwa ikiwemo kuangalia tume
iliyoundwa kama imezingatia vitu muhimu akiwemo muakilishi wa madereva
anayeaminika pamoja na tume hiyo kuwa ya uwazi huku akisisitiza kuwa,
endapo hadi kesho saa nne asubuhi ( Mei 6), tume hiyo haitakuwa na vitu
vya msingi, basi amewataka madereva kugoma tema na atawaunga mkono.
Na Andrew Chale, Modewji blog
Mgomo
uliodumu zaidi ya masaa 30, hatimaye leo Mei 5, majira ya Saa sita
mchana umemalizika na madereva kuingia kwenye magari yao na kuanza
safari kufuatia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Poul Makonda kujitoa
kafara kwa kuakikisha atasimamia madai yao yote muhimu yanashughulikiwa
kupitia tume iliyoundwa ndani ya masaa 19, huku akiwataka viongozi wa
madereva hao kuwa, hadi saa nne kesho endapo mambo hayatotimizwa basi
wafanye mgomo upya.
Makonda
alieleza kuwa, suala la tume ilioundwa na Waziri Mkuu ya watu 13,
kuzingatia mataakwa muhimu na ya msingi kwa madereva ambapo aliwaeleza
kuwa tume muhimu itahakikisha inashughulikia madai yao kwa muda wa siku 7
na kutoa majibu.
Akiongea
kwa kujiamini, Makonda aliwatangazia madereva haao wote kukiakikisha
hadi ifikapo kesho Mei 6, saa nne wawe wamejua haki zao za msingi
zimetekelezwa na kuzingatia ikiwemo kamati yao kuwa na mtu wanae mtambua
na kumuamini na pia tume hiyo iwe na habibu rejea na muelekeo wa ukomo
wake katika utekelezaji majukumu.
“HADI
KESHO SAA NNE ASUBUHI!!!! Endapo tume hiyo iliyoundwa haina mtu muhimu
wa madereva na munayemjua nyie kuwa hawezi kutatua matatizo yenu
munayodai, basi MUGOME NA MIMI NAWAUNGA MKONO TENA NAWAAMBIENI
WANANCHI, KESHO MISIKATE TIKETI MUKIONA HALI HAIJAWA SAWA KAMA MAMBO
YAO MADEREVA HAWAJATEKELEZEWA!” Alieleza Makonda na kushangiliwa na
umati huo wa madereva na wapiga debe.
Pia
Makonda alilitaaka jeshi la Polisi kutowasumbua kwa mabomu na mbwa
katika shughuli zao ikiwemo mgomo ambapo amewataka kukaa mbali na
madereva hao kwani nao wanadai haki zao za msingi.
Mwandishi Mwandamizi wa Modewji blog, Andrew Chale, akiendelea kuchukua matukio moja kwa moja..hatua kwa hatua wakati Makonda anaongea.
Mbunge
wa Hai, Moshi na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na ambaye ni
kiongozi mkuu wa UKAWA, Freeman Mbowe, akiongea machache katika mkutano
huo. Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Poul Makonda alishuka na
kipaza sauti na kutokomea nacho hali iliyozua tafrani kwa baadhi ya
madereva ambapo hata hivyo Mbowe alizungumza na madereva hao bila
kutumia kipaza sauti huku akishangiliwa muda wote. Mbowe alifika Ubungo
majira ya saa tano asubuhi na kushangiliwa na umati mkubwa wa madereva
hao.
Vijana wapiga debe. wakishangilia basi lililokuwa likitoka ndani ya kituo cha mabasi Ubungo kuelekea Mikoani
Umati wa watu ukiwa nje ukiangalia mabasi yaliyokuwa yakitoka kuanza safari zake nje ya geti la kuondokea mabasi ya mikoani
Basi linalofanya safari zake za Tanzania na Zimbabwe likitoka katika geti la stendi Ubungo kuanz safari zake…
Mmoja wa
vijana wanaofaya shughuli zao ndani ya kituo cha mabasi ubungo, ‘Chalii’
ambaye pia ni mdau mkubwa wa kuperuzi habari za mtandao ukiwemo
mtandao huu akiwa nje ya geti hilo akishuhudia mabasi hayo yaliyokuwa
yakitoka baada ya mgomo kuisha.
Umati ukiendelea kushuhudia mabasi yaliyokuwa yakitoka mapema mchana wa leo Mei 5 baada ya mgomo kumalizika
“MWANAUME
KAZINI’-Hali ya hewa ni baridi… lakini nilikuwa natokwa jasho baada ya
kazi ngumu ya kutafuta picha za matukio kupitia kifaa changu kidogo
yaani Pad ya Tecno P9, Namshukuru Mungu kwa hiki leo kwani hata huyo
mwenye camera kubwa na mimi sote tumepata picha na siku zinaenda. !!
Asante Mungu
Mwandishi
Mwandamizi wa mtandao huu, Andrew Chale aki-Selfie’ na baadhi ya wadau
wanaofanya shughuli zao katika kituo cha mabasi Ubungo muda mfupi baada
ya mgomo kumalizika katika geti la kutokea magari yaendayo mikoani na
nchi jirani.
Mwandishi
Mwandamizi wa mtandao huu Andrew Chale akipiga ‘selfie’ huku akiwa
ndani ya gari ndogo Cary ya 350gm, maarufu ‘Kilikuu’ akiondoka katika
eneo la Ubungo kurejea na majukumu mengine ya kitaifa kufuatia kupiga
kambi katika kituo hicho tokea asubuhi ya jana Mei 4 na kulala hapo hadi
leo Mei 5, majira ya saa saba mchana anareje kwenye majumu mengine
kufuatia kazi ngumu ya kuripoti mgomo huo.
0 comments:
Post a Comment