Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » ORIGINO KOMEDI WAKABIDHIWA MATREKTA YA KILIMO NA KAMPUNI YA FARM EQUIP TANZANIA JIJINI DAR LEO.

ORIGINO KOMEDI WAKABIDHIWA MATREKTA YA KILIMO NA KAMPUNI YA FARM EQUIP TANZANIA JIJINI DAR LEO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mwigizaji wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),akipewa maelekezo ya kuendesha Trekta mara Baada kukabidhiwa ufunguo wake na  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip Tanzania , Yunusu Nsekela wakati wa kukabidhiwa Matrekta kwaajili ya kilimo jijini Dar es Salaam leo
 Mwakilishi wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
 Mwakilishi wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink  akisalimiana mara baada ya akimkabidhi ufungua wa Trekta lake Mwigizaji wa Origino Komed, Isaya Mwakilasa(Wakuvanga) jijini Dar es Salaam leo.
  Mwigizaji wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee) akishukuru kwa niaba ya waigizaji wa kundi la Origino Komedi  mara baada ya kukabidhiwa Funguo za Matrekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink,Isaya Mwakilasa(Wakuvanga ),Lucacy Mhavile(Joti) na kulia ni Alex Chalamila(Mackregani).
  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akizungumza na Vijana wa Kundi la Origino    Komedi mara baada ya kuwakabidhi funguo za Matrekta ya kilimo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink , katika picha ya pamoja waigizaji wa kundi la Origino  Komedi na nyuma yao ni Matrekta ambayo wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano ya Matrekta ya Kilimo kati ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink na Waigizaji wa kundi la Origino Komedi, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Matrekta ya Kilimo ambayo waigizaji wa Kundi la Original Comedi wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
WAIGIZAJI wa kindi cha Origino Komedi  wamewaasa vijana kutumia vipaji vyao ili kutengeneza maisha yao kuwa  mazuri na sio kufikiri kuwa vijana wengi hushikwa mkono na mtu ili kufanikiwa.

Hayo yamesemwa na kundi la waigizaji wa Origino Komedi wakati wa kukabidhiwa Matrekta ya Kilimo aina ya Sonalika kutoka kampuni ya Farm Equip Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink amesema kuwa  vijana  wameamua kufanya jambo la maana kwa jamii ,"kwani wamenunua matrekta kwa ajili ya kilimo,vijana wengi wamekuwa wakinunua magari ya kifahari  bila kujua kunakesho na keshokutwa kwa maendeleo yao",alisema Bwa Arif.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewapongeza vijana wa kundi hilo kuwa kufanya maamuzi sahihi na ya maendeleo kwa kununua Matrekta hayo kwaajili ya kilimo,amesema kuwa uamuzi wao ni mzuri hata kwa jamii kwani pia kwa namna moja ama nyingine itasaidia kuongeza ajira kwa vijana,kwakuwa kilimo kinahitaji watu wengine na sio wao wenyewe watakao weza kuendesha Matrekta hayo mashambani.

Kundi hilo la Origino Komedi  linaundwa na vijana 7 ambao ni Alex Chalamila(Mackregani),Josef Shamba(Vengu),Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),Lucacy Mhavile(Joti), Isaya Mwakilasa(Wakuvanga),Emmanuel Mgaya(Masanja mkandamizaji) na Davidi Seki.

 Waigizaji hao wameahidi kupoleka Matrekta yao kwenda kubeba takataka katika Wilaya ya Kinondoni ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda atazindua  kampeni ya Ona aibu, ambayo itahamasisha usafi katika Wilaya ya Kinondoni.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa