Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Baa za Uwanjani Legho Zavunjwa

Baa za Uwanjani Legho Zavunjwa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Dagaa Dagaa (1)Mwanadada akiwa anaangalia vitu alivyofanikiwa kuviokoa.Dagaa Dagaa (2)Katapila likiendelea na kazi yake ya kubomoa .Dagaa Dagaa (3)Watu mbalimbali wakiwa kwenye vikundi wakijadili tukio hilo.Dagaa Dagaa (4)Eneo lililobomolewa.Dagaa Dagaa (5)Nyumba hizi mbili baadaye nazo zikabomolewa.Dagaa Dagaa (6)Dagaa Dagaa (7)Dagaa Dagaa (8)
BAADHI ya baa zilizopo katika viwanja vya Legho, Ubungo jijini Dar, leo zimevunjwa kufuatia agizo la mahakama kwa kile kilichodaiwa wamiliki walivamia eneo ambalo siyo lao.
Akizungumza na mwandishi wetu, dalali wa mahakama kutoka katika kampuni ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd, Elieza Mbwambo, alisema mmiliki halali  wa eneo hilo ni Dar Cool Makers Limited ambaye baada ya  kuvamiwa eneo lake alifungua kesi mahakamani mwaka 1993 ambapo iliendelea mpaka ilipofikia leo.
Wavamizi wa eneo hilo ambao ni John Ondoro Chacha, Jumuiya ya Wazazi CCM na mtu mwingine mmoja baada ya kuona mmiliki halali amepeleka kesi mahakamani nao wakaenda kuweka zuio ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru eneo hilo lirudi kwa mmliki halali ambapo wavamizi walitakiwa wabomoe vibanda walivyokuwa wamejenga walikokuwa wakifanya biashara ya baa.
“Januari 25 mwaka huu tulipewa oda na mahakama tuje kuwatoa hawa wavamizi, tuliweka tangazo kama wiki moja iliyopita lakini hawakujali hivyo leo ikawa ndiyo siku rasmi ya kuwaondoa na kama unavyoona ndiyo tunabomoa hivi.
“Mwenye kesi ya msingi ambaye ni John Ondoro Chacha alitakiwa kuwaambia wapangaji wake kwamba ameshindwa kesi lakini hakuwaambia ndiyo maana hata tangazo lilipowekwa hawakushtuka, kwa mujibu wa mahakama huyu Chacha ambaye kwa sasa ni marehemu na watoto wake ndiyo walikuwa wakipokea kodi ya kila mwezi kwa wafanyabiashara waliowapangia  wakati eneo hili siyo lao,” alisema Mbwambo.
Watu mbalimbali walionekana wakiwa wamesimama huku wakishangaa eneo hilo huku wengine wakilalamika kwamba watakuwa wanajiachia  wapi wakati walikuwa wamezoea viwanja hivyo.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za eneo la tukio:
PICHA, STORI: Na Gladness Mallya/GPL
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa