Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » LIFE FORMULA FAMILY MFUMO MPYA WA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KATIKA TASNIA YA SANAA

LIFE FORMULA FAMILY MFUMO MPYA WA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KATIKA TASNIA YA SANAA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

KAM1 
Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Dream Success Enterprises kwa kushirikiana  na kampuni ya Bid Production wameanzisha mfumo mpya wa kiuchumi ujulikanao kama “Life Formula Family (LFF)” kwa ajili ya kubuni masoko na mtaji katika tasnia ya Sanaa nchini.
Mfumo huo unatarajia kuzalisha wawekezaji Wazawa na Wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuipaisha sanaa ya Tanzania katika ngazi za kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bid Production, Bw. Fadhili alisema kuwa kampuni hiyo ina lengo la kuhamasisha wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuanzisha makampuni na kujiajiri na hivyo kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana.
Matekela alisema kuwa mfumo huo wa Life Formula Family unatarajia kuanza na Watu Milioni 5, ambapo mwanachama atakejiunga atapatiwa namba maalum ya utambulisho.. 
“Filamu zitakazoingizwa katika mfumo huu zinatarajiwa kuuzwa Tsh. 3,000 kwa wakazi wa jijini dare s salaam na kwa upande wa wakazi wa mikoani itategemea na gharama za usafirishaji” alisema Mateleka.
Aliongeza kuwa kampuni yake pia inatarajia kuendesha kongamano maalum lijulikanalo kama la “Sitaki kuajiriwa” ambalo litawahusisha wahitimu wa vyuo vikuu nchini, ambapo watajadiliana kwa pamoja tatizo la ajira kwa vijana na hatua za kukabiliana na tatizo hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Dream Success Enterprises, Charles Makoba alisema taasisi imeunga mkono kwa vitendo Hatua za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mkakati wa kutumbua majipu, hivyo taasisi yake imekusudia kutumbua jipu la ukosefu wa ajira kwa vijana.
“Tumeamua kuanzisha kampeni ya “Sitaki Kuajiriwa” kwa kuhimiza wahitimu na wanavyuo kuanzisha makampuni yao, na tayari kampuni ya kwanza ya Bid Production imeshajiliwa na tumeungana katika kuendesha kampeni ya Sitaki kuajiliwa” alisema Makoba.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa