Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu akutana na kufanya mazungumzo na Wasambazaji wa kazi za sanaa.

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu akutana na kufanya mazungumzo na Wasambazaji wa kazi za sanaa.

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Wawakilishi wa Wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini (hawapo pichani) waliotembelea kujua Urasimishaji wa kazi hizo katika ofisi ya Bodi hiyo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.


Afisa Utamaduni Bodi ya Filamu, Bw. Romanus Tairo akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Wawakilishi wa Wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini waliotembelea kujua Urasimishaji wa kazi hizo katika ofisi ya Bodi hiyo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Wahifadhi kazi za Sanaa, Bw. Frank Pangoni (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Kampuni ya Salt Inc, Bw. Edwin Musiba akifafanua (kulia) jambo mbele ya Wasambazaji kazi za Sanaa wakati wa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Wauzaji DVDs Mikononi, Bw. Jumanne China (kulia) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam katika ofisi hiyo.

Mwakilishi wa Wauzaji wa Jumla wa kazi za Sanaa, Bw. Augustino Karia (wa pili kushoto) akimweleza jambo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam katika ofisi hiyo.

 (Picha zote na Benedict Liwenga)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa