Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Boti
Jeupe lililonaswa na kikosi maalumu cha kuzuia uhalifu cha Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari (TPA) juzi wakati wahalifu wakijiandaa kutoboa
bomba na kuiba mafuta kwenye kina kirefu cha Bahari ya Hindi. Wahalifu
walifanikiwa kutokomea kusikojulikana baada ya kujitosa baharini, Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko
(kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb), kuhusu mafuta yanavyopakuliwa kutoka kwenye meli,
alipotembelea bandarini hapo ili kupata maelezo kuhusu mchakato wa
kupata mita mpya za kupimia mafuta (Flow Meters), Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko
(kushoto) akimuonesha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) (kulia), namna maharamia wa mafuta walivyoharibu miundombinu
ya bomba la mafuta baharini, baada ya kufanikiwa kukamata boti moja na
vifaa vyake lililokuwa likitumiwa na wahalifu hao kuiba mafuta.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwapongeza askari wa
doria waliofanikisha kukamata boti moja pamoja na vifaa vyake muhimu
ikiwemo injini baada ya kuwadhibiti maharamia waliotaka kutoboa bomba na
kuiba mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mmoja
wa maafisa wa TPA walioongoza zoezi la kupambana na wahalifu wanaoiba
mafuta kwenye bomba la mafuta akionesha vilipuzi vilivyokamatwa
vilivyokuwa vitumiwe na wahalifu waliokuwa wakijaribu kuiba mafuta
kwenye bomba la mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiangalia
baadhi ya vifaa ikiwemo injini ya boti, vilivyokamatwa baada ya wahalifu
kukurupushwa baharini wakijaribu kuiba mafuta kwa kutoboa bomba
baharini.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili
kulia)na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
(TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na wengine, walipotembela
Bandari ya Dar es Salaam, kitengo cha Mafuta, kukagua flow meters na
tukio la kukamatwa kwa boti lililokuwa likitumika kuhujumu bomba la
mafuta.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati),
akiwa juu ya mitambo ya kupitisha mafuta kutoka kwenye Meli alipokuwa
akipata maelezo ya namna Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, inavyodhibiti
mafuta ili Serikali ipate kodi yake stahiki.
Kaimu
Kamisha na Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Elijah
Mwandumbya, akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), kuhusu hatua zilizochukuliwa kudhibiti
upotevu wa mapato ya Serikali upande wa mafuta katika Bandari ya Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi
Deusdedit Kakoko, akitoa maelezo walipokuwa wakiagana na Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).Katika ziara hiyo Waziri
Mpango amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania na Mamlaka ya Mpato katika kudhibiti
ukwepaji kodi.
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdedit
Kakoko, ameiomba Serikali kuipatia Mamlaka yake vitendeakazi muhimu ili
kukabiliana na vitendo vya uharamia wa bomba la mafuta katika bahari ya
Hindi.
Mhandisi
Kakoko ametoa maombi hayo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, aliyetembelea bandari hiyo upande wa mafuta na kuelezwa kuhusu
tukio lililotokea juzi ambapo TPA wamekamata boti moja lilikuwa
likitumiwa na wahalifu kuiba mafuta kutoka kwenye bomba, baharini.
Katika
tukio hilo watu wasio fahamika, wakiwa na mabomu na baadhi ya vilipuzi,
walilitelekeza boti lao na kutoweka kusikojulikana kwa kupigambizi
baharini baada ya walinzi wa doria kuwakurupusha kwa kurusha risasi
hewani.
“Tunaomba
tupatiwe vitendeakazi kwa ajili ya kikosi chetu kinachofanyakazi kubwa
ya kupambana na uhalifu mbalimbali bandarini hasa magari ili kukiwezesha
kikosi hicho kufanyakazi yake kwa ufanisi” alieleza Bw. Kakoko
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameahidi kuipatia Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari vitendeakazi ambavyo viko ndani ya uwezo wake kama
Waziri ili kuongeza udhibiti wa eneo la maji ya bahari lenye bomba la
mafuta.
“Ninawapongenza
sana kwa kufanikisha kuwadhibiti maharamia hao ambao wamekuwa
wakitumika kuharibu miundombinu ya bomba na mafuta na kuharibu mita za
kupimia mafuta, nawaahidi kuwatimizia maombi yenu ya vifaa ambavyo viko
ndani ya uwezo wangu” alisema Dkt Mpango’
Alisema
kuwa vitendo vinavyofanywa na wahalifu hao vinakwamisha juhudi za
Serikali za kuimarisha miundombinu yake na kusabisha hasara kwa wenye
mafuta na kuikosesha Serikali mapato kutokana na vitendo hivyo vya
kutoboa bomba na kuiba mafuta.
Mbali
na kushuhudia boti lililokamatwa pamoja na vifaa vyake ikiwemo injini
na magaloni ya mafuta, Dkt, Mpango alipewa maelezo kuhusu mchakato
unaoendelea wa kufunga mita mpya za kupimia mafuta (flow meters).
Mhandisi
Kakoko ameeleza kuwa mchakato unaendelea vizuri na kwamba huenda
ukakamilika mapema mwakani hatua itakayosaidia kuongeza mapato ya
Serikali bandarini hapo.
0 comments:
Post a Comment