Na Mwandishi Wetu
KUNDI la muziki wa asili na dansi la Mambo
Safi limeanza kambi rasmi leo katika ukumbi wa Harbous Klab kwa ajili
ya kujiandaa na sherehe za Mei mosi zitakazofanyika katika ukumbi wa
Urafiki Club, Dar es Salaam.
Kundi hilo ambalo sambamba na kutoa burudani hiyo pia linajihusisha
na kucheza sarakasi pamoja na Ngonjera litakaa kambi hiyo kwa muda wa
wiki moja ili kuweza kujiimarisha.
Akizungumza Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi wa SF group Camponies ltd ambayo ndio inasinamia kundi hilo
Selina Koka alisema katika kambi hiyo watakuwa wakifanya mazoezi katika
burudani zote wanazozitoa.
"kundi hili huwa linatoa burudani katika shughuli mbalimbali za
kiserikali na hii ni moja ya shughuli za kiserikali na ndio maana
tumeamua kuweza kambi ili kuweza kujiandaa vya kutosha kwa ajili ya
kusheherekea siku hiyo," alisema.
Aliongeza kuwa kundi hilo ambalo linajumla ya wanamuziki 22
linatarajia kuanza kutoa burudani kwa kila wiki katika ukumbi tofauti
kama zilivyobendi nyingine ili kuweza kutoa burudani zaidi.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo Phabbian Salvatory 'Super Phabby'
alisema wanaliandaa kundi hilo kutoa upinzani kwa bendi nyingine kongwe
kama Extra bongo, Twanga na nyinginezo ili kuweza kujiweka katika ramani
nzuri ya muziki wa dansi hapa nchini.
"hatutaki kuishia hapa tunataka kuwa kama bendi nyingine na hata
tuwashinde kwa kuwapa upinzani mkubwa ili kuweza kuwaonyesha uwezo wetu
tulionao," alisema.
0 comments:
Post a Comment