Home » » Simba sasa safari nyeupe Ubingwa wa Tanzania Bara Baada ya kushinda Goli 3 bila dhidi ya JKT Ruvu

Simba sasa safari nyeupe Ubingwa wa Tanzania Bara Baada ya kushinda Goli 3 bila dhidi ya JKT Ruvu



Mchezaji Uhuru Selemani wa timu ya Simba kushoto akishangilia goli la kwaza alilofunga dhidi ya timu ya JKT Ruvu pamoja na na wachezaji wenzake Gervas Kago kulia na Patrick Mafisango, Simba inacheza na JKT Ruvu kwenye uwanja wa Taifa jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ambapo Simba leo imeibuka kidedea kwa goli 3-0, goli la pili likifungwa na mchezaji Haruna Moshi "Boban", huku la tatu lililowageuza nyuma maafande hao wa JKT likipachika wavuni na Mwinyi Kazimoto. 


Mchezo wa leo umeihakikishia Simba kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka tanzania Bara mwaka huu hasa kutokana na matokeo mabaya ya waliokuwa wapinzano wao Yanga ambayo leo tena imecharazwa bakora moja ya muwa na vijana wa Kagera Sugaer.
 Mashabiki wa Timu ya Simba wakishangilia kwa nguvu baada ya timu yao kujipatia magoli dakika za mwanzomwanzo za mchezo huo.
Picha na Full Shangwe Blog.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa