Baadhi ya walimu na wafanyakazi wa Taasisi ya HakiElimu wakionesha mabango mbalimbali
kwa wanahabari kuhamasisha elimu ya awali.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Awali ya Mchangani iliyopo jijini Dar es
Salaam wakionesha bango lenye ujumbe juu ya maboresho ya elimu ya awali.

Mkurugenzi
Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia, akigawa zawadi ya vifaa
anuai vya masomo kwa wanafunzi wa shule ya awali ya Mchangani mara baada
ya uzinduzi huo.

Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia (mwenye blauzi nyekundu)
akigawa zawadi ya vifaa anuai vya masomo kwa wanafunzi wa shule ya awali
ya Mchangani mara baada ya uzinduzi huo.

Na Joachim Mushi
TAASISI ya HakiElimu imezindua matangazo mapya ya
redio na televisheni ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha jamii na Serikali
juu ya umuhimu wa elimu ya awali kwa watoto kabla ya kujiunga na darasa
la kwanza. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za
HakiElimu na kuhudhuriwa na baadhi ya walimu na wanafunzi wa awali,
waandishi wa habari, wadau mbalimbali wa sekta ya elimu, pamoja na
malezi na makuzi ya watoto.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi.
Elizabeth Missokia alisema shirika hilo lemeamua kuzindua kampeni hiyo
iliyopewa jina la “Boresha Elimu ya Chekechea” lengo kuu likiwa ni
kuitaka Serikali itimize ahadi na wajibu wake wa kutoa elimu bora kwa
wanafunzi wote wa elimu ya awali.

Mkurugenzi huyo alisema elimu ya awali kwa mtoto ni muhimu sana
katika kujenga msingi imara kielimu na endapo elimu hiyo itatolewa
kikamilifu, inakuwa ni msingi imara kwa mtoto katika elimu yake ya
baadae na pia elimu hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kimwili,
kiakili na kimaadili.

“Katika Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 1995 Serikali inaonesha
umuhimu wa elimu ya awali, inapotamka; ‘Tafiti kadhaa zilizofanyika
nchini katika miaka ya 1980 zilibaini kuwa watoto waliopitia elimu ya
awali huwa na mafanikio makubwa zaidi wanapoanza darasa la kwanza.
Kutokana na kutambua umuhimu huu, Serikali iliamua kuingiza Elimu ya
Awali kwa watoto wenye umri wa miaka 5 na 6 kwenye mfumo rasmi wa elimu
na kila shule ya msingi inapaswa kuwa na madarasa ya Elimu ya Awali’,”
alisema Missokia.

Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni hii HakiElimu imefanya tafiti
katika sehemu mbalimbali nchini na kubaini hali ya utoaji wa elimu ya
awali na mazingira yake inatia huruma kwani elimu hiyo inavyotolewa
katika mazingira yasiyofaa jambo ambalo linachangia kushuka kwa kiwango
cha elimu nchini.

“Kama ilivyo katika elimu ya msingi na ile ya sekondari, elimu ya
awali imegubikwa na changamoto nyingi. Baadhi ya changamoto hizi ni
upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, unaosababisha mrundikano mkubwa
katika madarasa, ukosefu mkubwa wa walimu wenye taaluma ya elimu ya
awali pamoja na vifaa vya kufundishia. Aidha, kutokuwepo na tofauti ya
kimadarasa katika elimu ya awali (yaani watoto wa umri wa miaka 5 na
miaka 6 kusoma katika darasa moja), na wingi wa masomo pia ni
changamoto,” alisema.

Aidha aliongeza kuwa licha ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru Kawambwa, katika makadirio na matumizi ya wizara yake ya
mwaka 2012/13, kukiri kuwa Serikali imetoa mwongozo kwa kila shule ya
Msingi kuwa na darasa la Elimu ya Awali, lenye madawati yanayolingana na
hali ya watoto wa elimu hiyo, kujenga vyoo kwa ajili ya watoto wa Elimu
ya Awali wasiingiliane na wale wa shule za msingi, lakini bado kuna
mapungufu makubwa katika utekelezaji wake.

“Baada ya kuona madhara ya kukosa elimu bora ya awali kwa watoto
wetu, HakiElimu inatoa wito kwa watanzania wote nchini wenye mapenzi
mema na maendeleo ya taifa letu kuungana nasi katika kampeni hii kwa
njia zifuatazo; Kuhimiza wananchi wote wenye watoto wenye umri wa
kuandikishwa shule za awali wafanye hivyo kwa wingi. Kuna baadhi ya
sehemu inaripotiwa wazazi bado hawajaelewa umuhimu wa kuwapeleka watoto
katika madarasa haya ya awali.

“Kuwabana viongozi wetu tuliowachagua kuanzia mwenyekiti wa mtaa,
diwani na Wabunge wetuwanachukua hatua kukabiliana na changamoto
zilizopo ili kufanikisha Elimu bora ya Awali kwa watoto wetu.

Wananchi kuandika barua kwenye magazeti mbalimbali hapa nchini
zikielezea hali ya elimu ya awali inavyotolewa katika maeneo mliyopo.”
HakiElimu imeshauri barua zinazoandaliwa na wananchi kuzituma moja
kwa moja kwa Wahariri wa magazeti wanayoyasoma kupitia anuani zilizopo
katika gazeti husika, au wanaweza kuzituma kupitia sanduku la barua
79401 Dar es Salaam zikiwa na kichwa cha habari ‘BORESHA CHEKECHEA’,
ambapo HakiElimu itafanya kazi ya kuzipeleka katika magazeti mbalimbali
nchini.

Aidha, ili kuchagiza mafanikio katika sekta ya elimu, HakiElimu
imeandaa vipindi vya radio katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Tabora,
Tanga, Kagera, Dodoma na Mara ambavyo vitatoa nafasi ya Marafiki wa
Elimu kujadili jinsi gani elimu ya awali inaweza kuboreshwa.

Hata hivyo kwa Watanzania wanaotumia mtandao wa ‘Internet’ wanaweza
kushiriki kampeni hii kwa kutembelea; www.facebook.com/hakielimu,
www.twitter.com/hakielimu na www.hakielimu.blogspot.com.

No comments:
Post a Comment