Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » DKT. CHARLES MWIJAGE AITAKA NBS KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO KUFANYA TAFITI YA VIWANDA VIDOGO NCHINI

DKT. CHARLES MWIJAGE AITAKA NBS KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO KUFANYA TAFITI YA VIWANDA VIDOGO NCHINI


nba6
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba1
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba2
Baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba4
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (katikati) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau mbalimbali wakati uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
nba5
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba7
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba8
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu mbalimnbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
nba9
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto) akimkabidhi taarifa ya kitabu cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
 
                                                Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-Dar es Salaam

SERIKALI imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini NA Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.

Dkt Mwijage alisema kuwa katika mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.

Alisema katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia kuinua uchumi wan chi.

“Asilimia 25- 40 ya mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao yao” alisema Mwijage.

Aidha, Dkt Mwijage alisema, sekta ya viwanda vidogo vidogo nchini imeendelea kukua kwa kasi nchini ambapo hadi sasa kuna jumla ya viwanda 3800 vilivyoanzishwa nchini kuanzia Novemba 2015 hadi octoba, 2016.

Katika hatua hiyo Dkt Mwijage alisema kuwa Wizara yake inaendelea kuhamasisha Sekta binafsi kuwekeza katika Sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ikiwa jukumu kuu la Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na inajenga mazingira wezeshi kwenye sekta binafsi kuzalisha na kufanya biashara.

Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alisema kuwa matokeo hayo yanaonyesha mafanikio katika sekta ya viwanda ikiwemo kuongezeka kwa ajira zipatazo 264,223 nchini na kuchangia uchumi kwa takribani Shilingi bilioni 8.0 kwa mwaka 2013.

Alisema kuwa Takwimu za matokeo ya sense ya uzalishaji viwandani ni rasmi na kuwataka watunga sera, wanasiasa, viongozi, sekta binafsi na watu binafsi kutumia matokeo hayo kwa lengo la kuboresha Sekta ya viwanda nchini.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa