Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » HAFLA YA UTILIAJI SAINI MIKATABA 21 KATI YA TANZANIA NA MORROCO

HAFLA YA UTILIAJI SAINI MIKATABA 21 KATI YA TANZANIA NA MORROCO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwa ajili ya kumpokea Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa ulinzi wakati wa kumpokea Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco kwa ajili ya hafla utiaji saini wa mikataba 21 kati ya Tanzania na Morocco.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwaeleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco mara baada ya kuwasili Ikulu leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla utiaji saini wa mikataba 21 kati ya Tanzania na Morocco.

Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco Akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco wakiwaangalia wapigaji ngoma mara baada ya kuwasili Leo Ikulu Jijiji Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco wakipiga ngoma mara baada ya kuwasili Leo Ikulu Jijiji Dar es Salaam.

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 21 kati ya Tanzania na Morocco.

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustino Mahiga akiizungumzia mikataba 21 itakayosainiwa kati ya Tanzania na Morocco.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akieleza namna Tanzania itakavyonufaika na mikataba 21 iliyosaniwa katika ya Nchi ya Morocco na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano ya Morocco Bw. Salahddine Mezouar akimueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli sababu za kuja kuwekeza Tanzania Ikiwamo utulivu wa Kisiasa na ushirikiano wa Muda mrefu.
Mwenyekiti wa shirikisho la wafanyabiashara wa Morocco Bi. Miriem Bensalah akiongea na kwenye hafla utiaji saini ambapo wamekubaliana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania kuanzisha Baraza la Biashara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano ya Morocco Bw. Salahddine Mezouar na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustino Mahiga wakisaini moja ya mikataba 21 leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano ya Morocco Bw. Salahddine Mezouar na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustino Mahiga wakibadilishana mikataba leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Sekta binafsi Tanzania pamoja na wenzao wa Morocco wakisaini na kubadilishana mikataba leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na viongozi wa serikali na sekta binafsi wa Tanzania na Morocco wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba 21 kati ya Tanzania na Morocco.
Picha na Hassan Silayo


Na Daudi Manongi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na Mfalme Mohamed  wa Sita  wa Morocco kujenga Uwanja wa Mpira wa miguu wa  kisasa mkoani Dodoma utakaogharimu dola milioni 100.


Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kutiliana saini kwa mikataba 21 ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Morocco.


“Mbali na mikataba baina ya Tanzania na Morocco nimezungumza mambo mbalimbali na Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco na nimemuomba atujengee Uwanja mkubwa wa mpira pale Makao Makuu yetu Dodoma utakaokuwa na thamani kati ya dola milioni 80 hadi  100 na amesema ataujenga, kwa hiyo utakuwa Uwanja mkubwa kuliko wa Dar es Salaam”. Alisema Rais Magufuli.


Mbali na hayo Rais Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara wa Morocco kuwa Tanzania ni salama na inapenda kushirikiana nao, na kuwa nchi yetu iko katika mwelekeo mzuri wa uwekezaji ambapo uchumi wa nchi yetu unategemea kukua kwa asilimia 7.2 mwishoni mwa mwaka.


Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw.Salahddine Mezour ameishukuru nchi ya Tanzania kwa ushirikiano iliounyesha na kusema kuwa Morocco itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali kwa kuwa ina utulivu wa kisiasa na icho ndo kimekuwa kivutio kikubwa katika kuwekeza kwao nchini hapa.


Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais, Dk John Pombe Magufuli ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili na kutiliana saini mikataba 21 ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa