Na Mwandishi Wetu Dodoma
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter
Serukamba ametoa wito kwa wadau wa Habari kuendelea kutoa maoni yao
kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kamati yake.
Aliongeza
kuwa kwa sasa kamati yake inaendelea na kazi ya kuujadili Muswada wa
Sheria ya Huduma za Habari kwa kuendelea kupitia kifungu kwa kifungu na
baadae kuunganisha na maoni ya wadau ambayo hayapo kwenye Muswada huo
kabla ya kuupeleka kujadiliwa Bungeni.
“Nitoe
tu wito kwa wadau wa Habari kuzidi kuto maoni yao kuhusu Muswada huu
kwani wao ndio wahusika wakuu wa Sheria hii ” alisisitiza Mhe.
Serukamba.
Mhe.
Serukamba amesisitiza kuwa wadau wa habari na wanahabari wanapaswa
kufahamu kuwa Muswada huo utaleta Sheria iliyo bora kwa mufaa ya tasnia
ya habari na watanzania kwa ujumla.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau habari kupitia barua pepe ya cna@bunge.go.tz.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment