Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI KUWANUFAISHA JAMII

MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI KUWANUFAISHA JAMII

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Lorietha Laurence-WHUSM
Mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliwasilisha kwa mara ya kwanza Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari Bungeni Mjini Dodoma.
Tangu kuwasilishwa kwa Muswada huo kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa wadau habari ni kwa namna gani  jamii na tasnia ya habari na itanufaika na Sheria hiyo.
Mmoja wa wadau wa habari Bw. Malekela Maingu katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii alihoji endapo Muswada huu upo kwa ajili ya kunufaisha wanahabari peke yake, swali ambalo wadau wengi watakuwa wakijiuliza.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari upo kwa ajili ya watu wote kwa kuwa katika Muswada huo umezingatia kumlinda mwandishi na mwananchi kwa kutoa habari za uhakika ili kuzuia mgawanyiko kwa jamii endapo itatokea kashfa.
Katika sehemu ya Tano kifungu cha 32(1) cha Sheria hii inaeleza kuwa jambo lolote kama likichapishwa au kutangazwa  linaweza kuharibu sifa ya mtu kwa kumfanya achukiwe, adharauliwe au  afanyiwe kejeli au linaweza  kumharibia mtu kazi yake kwa kuchafua jina  lake au kumvunjia heshima yake jambo hili litahesabika kuwa ni kashfa.
Kufuatia kifungu hicho ni wazi Sheria hii itasimamia haki ya mtu endapo taarifa zitakazotolewa kuhusu mtu huyo  zitabainika  kuwa ni za uongo zenye nia ya kumchafulia jina ama kumdhalilisha.

Kifungo hicho kinaendelea kueleza  kuwa Sheria hii  inamtaka mwandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi kwa kutoa taarifa zilizo za kweli na zenye uhakika ili kulinda maslahi ya nchi na watu wake.
Naye Bw. Amour Kagya ameipongeza Serikali kwa kuleta Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na kueleza kuwa kupitia Sheria hii kazi ya uandishi wa habari itaheshimiwa na kuthamaniwa.
Bw. Kagya amesema wanahabari watanufaika kwa uwepo wa mfuko wa mafunzo ya habari kwani utawasaidia kujiendeleza na kukuza tasnia ya uandishi wa habari hivyo kuipa hadhi fani hiyo.
Mwisho.



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa