Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa kwa sasa ina ndege tatu, zikiwemo mbili mpya aina ya Dash8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abira 76 kila moja na Dash8-Q300 moja yenye uwezo wa kubeba abiria 50.
Ndege hizo zinaendelea kufanyiwa ukaguzi na mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA). Zoezi hilo litakapokamilika kutakuwa na mazoezi ya vitendo kwa marubani na wafanyakazi wengine wa ndani ya ndege. Safari za biashara za kuruka na abiria zinatarajiwa kuanza tarehe 15 Oktoba 2016 na zitafanyika kwenye viwanja vifuatavyo:- Mwanza, Arusha, Zanzibar, Kigoma, Tabora, Mbeya, Mtwara, Kilimanjaro, Bukoba, Dodoma na Mpanda - nchini. Nje ya nchi yetu ATCL itaruka kwenda Comoro, Nairobi na Entebbe.
Aidha, ATCL inachukua fursa hii kuwaomba wadau wake wote kuwa na subira wakati tukiendelea kusubiri taratibu za mamlaka ya usafiri wa anga zikamilike.

Imetolewa na;

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI
AIR TANZANIA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa