Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TABATA KIMANGA JIJINI DAR ES SALAAM WAOMBA KUONDOLEWA TAKATAKA BARABARANI

TABATA KIMANGA JIJINI DAR ES SALAAM WAOMBA KUONDOLEWA TAKATAKA BARABARANI


 Mchuuzi wa mbogamboga akipita karibu na takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na kituo cha daladala cha Tabata Kimanga mwisho Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
 Takataka zikiwa kando ya barabara.
Mwendesha bodaboda akizikwepa takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na stendi ya daladala ya Tabataaa Kimanga mwisho jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Dar es Salaam juzi mkazi wa eneo hilo, Mfaume Wakwetu alisema katika maeneo mengi ya Tabata Kimanga kunatakataka nyingi zimerundikwa kando ya barabara bila kuondolewa na wahusika.

"Takataka nyingi zimerundikwa katika eneo la stendi ya mabasi hapa Tabata Kimanga na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa stendi hiyo na wapita njia" alisema Mfaume.

Aliongeza kuwa takataka zilitolewa majumbani huwekwa katika madampo madogo yaliyoanzishwa kandio ya barabara lakini mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hushindwa kufika kwa wakati kuziondoa hivyo kuwa kero kwao.

Aliongeza kuwa kutokana na takataka hizo kuachwa kwa muda mrefu bila kuondolewa husambaa hadi kwenye mifereji ya maji taka ambayouziba na kusababisha maji kushindwa kupita na kutoa hahrufu kali na kusababisha mafuriko mvua zinaponyesha.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa